Mhe.Victor Kawawa akichangia hoja juu ya Muswada wa sheria
ya udhibiti wa Ajira za wageni wa mwaka 2014 uliyosomwa na Waziri wa Kazi na
Ajira Mhe. Gaudensia Kabaka, leo bungeni Mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Janet Mbene akijibu
swali la Mhe.Philipa Mturano Mbunge wa viti maalum lililokuwa likihoji ni namna
gani Serikali imejipanga kuthibiti biashara ya vyuma chakavu kutokana na kuwepo
na wizi wa mabomba.
Waziri
wa Kazi na Ajira Mhe.Gaudensia Kabaka akisoma muswada wa sheria ya Udhibiti wa
Ajira kwa Wageni ya mwaka 2014 kwa mara ya pili ndani ya Bunge, leo Mjini,Dodoma
Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe.Aggrey Mwanri akijibu swali la
Mhe. Dkt Festus Limbu Mbunge wa Magu,lilikuwa likihoji ni kiasi gani cha kodi
ya Majengo kimekusanya katika kipindi cha miaka mine na nusu ya kwanza ya mwaka
wa fedha wa 2014/2015.
Waziri wa Fedha Mhe.Saada Mkuya (kushoto) akizungumza na
Wizara wa Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Mhe.Fenella Mukangara nje ya Ukumbi wa Bunge mara baada ya kikao, Mjini
Dodoma.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia
Mhe.January Makamba (kulia)pamoja na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe.Zitto Kabwe(kushoto)
wakifurahi pamoja na Walimu na Wanafunzi kutoka Shule ya Msingi ya Dar es Salaam Independent nje ya Bunge mara baada
ya kikao cha bunge, leo, Mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment