Habari za Punde

Mahafali ya sita ya chuo cha Uandishi wa Habari Zanzibar


 Baadhi ya wahitimu wa chuo cha Uandishi wa Habari Zanzibar ngazi ya cheti na stashahada wakiwa katika mahafali ya sita ya kumaliza mafunzo yao yaliyofanyika katika viwanja vya Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Kikwajuni Mjini Zanzibar.

 Mhitimu wa Chuo cha Uandishi wa Habari Zanzibar Aboubakar Harith Bakari akisoma Risala ya wanachuo wenzake katika mahafali ya Sita ya chuo cha uandishi wa Habari Zanzibar.

 Wahitimu wa Chuo cha Uandishi wa Habari Zanzibar ngazi ya Stashahada wakihudhurishwa kupatiwa Stashahada zao baada ya kumaliza mafunzo yao.

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akimpatia tuzo mwanafunzi Tabia Abdi Amour aliyefanya vizuri zaidi katika somo la Uandishi wa Magazeti { Print in Journalism } ngazi ya Diploma.
Kushoto ya Balozi Seif ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mh. Said Ali Mbarouk.

 Balozi Seif  huo cha akimpongeza Mkuu wa Chuo cha Uandishi wa Habari Zanzibar Dr. Aboubakar Sheikh Rajab mara baada ya kumalizika kwa mahafali ya sita ya chuo cha Uandishi wa Habari Zanzibar yaliyofanyika katika Viwanja vya Wizara ya Habari Kikwajuni Mjini Zanzibar.
Mbele ya Balozi Seif ni Waziri wa Habari Mh. Said Ali Mbarouk, nyuma ya Balozi ni Mwenyekiti wa Braza la Chuo cha Uandishi wa Habari Nd. Chande Omar Omar na Naibu Waziri wa Habari Mh. Bihindi Hamad.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyevaa joho rangi ya zambarau aliyesimama pembeni kushoto akiambatana na Waziri wa Habari,Utamaduni, Utalii na Michezo Mh. Said Ali Mbarouk kulia yake pamoja na Mkuu wa Taaluma wakiyapokea maandamano ya wahitimu 105 wa cheti na Stashahada wa Chuo cha Uandishi wa Habari Zanzibar waliomaliza mafunzo yao mkupuo wa sita.



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.