Timu zinazoshiriki michuano ya Afrika Mashariki wakiingia katika kiwanja cha Gymkhana kwa maandamano wakati wa ufunguzi wa Michuano hiyo leo jioni.Timu ya Mafunzo ikiingika katika viwanja hivyo.
Timu zinazoshiriki michuano ya Afrika Mashariki wakiingia katika kiwanja cha Gymkhana kwa maandamano wakati wa ufunguzi wa Michuano hiyo leo jioni.Timu yaKenya ikiingika katika viwanja hivyo.
Timu zinazoshiriki michuano ya Afrika Mashariki wakiingia katika kiwanja cha Gymkhana kwa maandamano wakati wa ufunguzi wa Michuano hiyo leo jioni.Timu ya Zimamoto ikiingika katika viwanja hivyo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mhe Said Ali Mbarouk, akiwa na Viongozi wa Vyama vya Mpira wa Netiboli wakisimama wakati ukipingwa Wimbo wa Afrika Mashariki wakati wa Ufunguzi wa Michuano hiyo leo katika viwanja vya Gymkhana.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Pete Zanzibar (CHANEZA) Ndg. Saadun Ahmeid, akitowa maelezo ya maandalizi ya Michiuno hiyo wakati wa ufunguzi uliofanywa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar Mhe Said Ali Mbrouk.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Netiboli Zanzibar ( CHANEZA ) Bi Mkemimi Muhina, akisoma taarifa ya kukamilika kwa michuano hiyo wakati wa ufunguzi wake na kutowa shukrani kwa wafadhili waliojitokeza kuyafadhili mashindano hayo na kufanikiwa kufanyika Zanzibar leo katika viwanja vya Gymkhana Zanzibar, na kufunguliwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar Mhe Said Ali Mbrouk.
Mwenyekiti wa Chama cha Netiboli Afrika Mashari Anna Kibira, akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Michuano hiyo ya Netiboli ya Afrika Mashariki katika viwanja vya Gymkhana leo jioni .
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar Bi Shery Khamis, akizungumza katika sherehe za ufunguzi wa Michuano ya Netiboli ya Afrika Mashariki yanayofanyika Zanzibar katika viwanja vya Gymkhana, kwa Ufunguzi wa michezo miwili kati ya Timu ya JKU na KVZ, Timu ya JKU imeshinda 40-27. na mchezo wa Ufunguzi kati ya Mabingwa Watetezi wa Kombe hilo timu ya Bima ya Uganda imecheza na Zimamoyo, Timu ya Bima ya Uganda (NIC) Imeshinda 62--21.
Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Mhe Said Ali Mbarouk, akizungumza na Wanamichezo wa Timu shiriki za Michuano ya Afrika Mashari ya Mchezo wa Netiboli na kutowa nasaha zake kwa washiriki kutumisha urafiki wa Nchi shiriki na kuahidi zawadi timu itakayochukuwa Ubingwa Mwaka huu.
Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Mhe Said Ali Mbarouk, akifungua michuano ya Afrika Mashariki kwa kurusha mpira golini ikiwa ni ishara ya uzinguzi wa michuano hiyo iliofanyika katika viwanja vya Gymkhana Zanzibar kwa mchezo wa Ufunguzi kati ya Timu ya Bima ya Uganda (NIC) na Timu ya Kikosi cha Zimamoto kwa upande wa Wanawake timu ya NIC imeshinda 62--21 na kwa Upande wa timu za Wanaume imezikutanisha timu ya JKU na KVZ, Timu ya JKU imeshinda 40-27, michuano hiyo inafanyika katika uwanja wa Gymkhana Zanzibar.
Kikosi cha timu ya Bima ya Uganda (NIC) ni Mabingwa Watetezi wa Kombe hilo la Afrika Mashariki imeweza kutetea Ubingwa wake kwa kuifunga Timu ya Zimamoto kwa mabao 62--21. wakati wa mchezo wake wa ufunguzi wa michuano hiyo iliofanyika katika kiwanja cha Gmykhana leo jioni 14-3-2015.
Kikosi cha Timu ya Kikosi cha Zimamoto Zanzibar kilichokubali kipigo kutoka kwa Mabingwa Watetezi wa Michuano hiyo Timu ya Bima ya Uganda, kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wao wa ufunguzi kuaza
Wachezaji wa NIC na Zimamoto wakiwania mpira wakati wa mchezo wao leo jioni uliofanyika katika viwanja vya gmykhana,Timu ya NIC ya Uganda imeshinda 62-21.
Mchezaji wa timu ya Zimamoto akiwa na mpira akijiandaa kutowa pasi.
Wachezaji wa Timu ya NIC na Zimamoto wakijiandaa kudaka mpira wakati wa mchezo wao wa ufunguzi wa michuano ya Kombe la Afrika Mashariki inayofanyika Zanzibar katika viwanja vya Gmykhana.
No comments:
Post a Comment