Mafundi wakiendelea na ufungaji
wa transfoma katika kituo kipya cha mtambo wa gesi wa kuzalisha umeme
(Kinyerezi 1) kwa awamu ya kwanza ujenzi unaotarajiwa kukamilika mwaka huu.
Kituo hicho kitakua na uwezo wa kuzalisha umeme wa Megawatt 150.
Baadhi ya watendaji wa ZECO wakipata maelezo ya ujenzi wa kituo cha mtambo wa gesi wa kuzalisha umeme (Kinyerezi 1) kinachoendelea kujengwa huko Kinyerezi Dar es Salaam. Baada ya kukamilika ujenzi wake kwa awamu ya kwanza kituo hicho kinatarajiwa kuzalisha umeme wa Megawatt 150 ambao utasambazwa baadhi ya maeneo na mwengine kuingizwa kwenye gridi ya taifa.
Watendaji wa ZECO wakitoka katika kituo cha mtambo wa gesi wa kuzalisha umeme Ubungo jijini Dar es Salaam – nyuma ndio kituo chenyewe.
Watendaji wa ZECO wakipata maelezo jinsi gesi inavyosanifiwa hadi kuzalishwa umeme na kuingizwa kwenye gridi ya taifa katika kituo cha mtambo wa gesi wa kuzalisha umeme Ubungo jijini Dar es Salaam.
Mhandisi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) akitoa maelezo ya kiusalama kwa watendaji wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) kabla ya kuingia kwenye mitambo ya uzalishaji umeme wa gesi katika kituo cha mtambo wa gesi wa kuzalisha umeme Ubungo jijini Dar es Salaam.
Watendaji wa Shirika la Umeme
Zanzibar (ZECO) wakipata maelezo ya kiufundi kupitia komputa jinsi ya
uzalishaji na usambazaji umeme unaotokana na gesi asilia.
Ujumbe wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) umefanya
safari kuelekea Tanzania Bara kwa lengo la kujifunza mambo mbali mbali ya
uzalishaji, usambazaji na ugavi wa umeme katika Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO). Pamoja na kujifunza huko ziara hiyo vile vile ina lengo la kukuza
mahusiano mazuri na mashirikiano katika nyanja mbali mbali za kirafiki pamoja
na kiufundi.
No comments:
Post a Comment