Habari za Punde

BAN KI MOON AWAGEUKIA VIONGOZI WA MADHEHEBU YA DINI DUNIANI

Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Tuvako Manongi akichangia wakati wa mkutano huo, ambapo  pamoja na mambo mengine alielezea uzoefu wa Tanzania ambao ni ule wa  viongozi wa madhehebu ya kiislam na kikikristo wa kukaa  pamoja na kujadiliana changamoto mbalimbali pamoja na  kuzitafutia ufumbuzi kupitia umoja wao. vile vile akasema kwamba jitihada za kukabiliana na  changamoto zitokanazo na itikadi kali za kidini na ukereketwa wa kupindukia  zinatakiwa zifanywa na kumilikiwa  na nchi husika pasipo kuingiliwa na mataifa kutoka nje. Aidha amesisitiza haja  na umuhimu wa  kuangalia na kutafutia ufumbuzi  matatizo ya kiuchumi na kijamii ambayo yanawafanya  vijana ambao wanakosa fursa ya kuendesha maisha yao kujiingiza katika vitendo vinavyokwenda kinyume na  maadili ya  kidini au ya utaifa.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban  Ki Moon akiwa na  Viongozi wa Madhehebu  mbalimbali ya Dini mara baada ya  viongozi hao wa dini kuzungumza katika mkutano wa ngazi ya juu uliojadili  pamoja na mambo mengi kuongezeka kwa vurugu zitokanazo na itikadi kali za kidini na ukereketwa wa kupindukia na  nini kifanyike kukabiliana na  changamoto hiyo. katika picha hii yupo pia Rais wa Baraza Kuu la  Umoja wa Mataifa, Bw. Sam Kutessa ambaye ndiye aliyandaa mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.