Waziri wa Ardhi Maji Nishati na Makaazi, Mhe Ramadhani Abdalla Shaban akizungumza na Wanawanchi wanaoishi katika Nyumba za Maendeleo Unguja ambo wamepewa nyumba hizo na Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, Akitowa tamko kuwa kwa wale waliopewa nyumba hizo na Mzee Karume wataendelea kukakaa katika nyumba hizo bila ya kulipa Kodi na wale waliorithi kwa Wazazi wao watalipa Kodi ya nyumba hiyo. mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa jengo la sanaa rahaleo Zanzibar.
Wakaazi wa nyumba za maendeleo Zanzibar wanaoishi katika nyumba hizo walizopewa na Mzee Karume wakiwa katika mkutano huo na Waziri na Viongozi wa Idara ya Nyumba Zanzibar kupata muafaka waka wa suala lao.
Viongozi wa Wizara ya Ardhi wakimsikiliza Waziri Shabani akizugumza wakati wa mkutano huo. wakwanza Mkurugenzi wa Idara ya Nyumba Ndg Abdalla Mwinyigogo na Naibu Waziri wa Wizara hiyo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Ndg Mustafa Aboud Jumbe na Mama Fatma Karume wakifuatilia mjadala wakati wa mkutano huo na Wakaazi wa Nyumba za Maendeleo Zanzibar waliopewa na Marehemu Mzee Karume.
Wakaazi wa nyumba hizo wakifuatilia mjadala huo.
Mama Fatma Karume akizungumza wakati wa mkutano huo wa wananchi waliopewa nyumba kwa ajili ya makaazi na Marehe Mzee Karume kwa makaszi yao
Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakifuatilia mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa jengo la sanaa rahaleo Zanzibar.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardh Zanzibar Ndg Mustafa Aboud Jumbe akizungumza wakati wa mkutano huo na Wananchi waliopewa nyumba za Maendeleo na Mzee Karume kupata ufumbuzi wa matatizo yao waliokuwa wakidai kwa Wizara.
Waakaazi wakifuatilia Mkutano huo na Waziri Shabani.
Ustadh. akisoma dua baada ya kumalizika kwa nmkutano huo uliowakutanisha Wananchi wanaokaa nyumba za Maendeleo waliopewa na Mzee Karume kwa kuishi Zanzibar.
AHH..HII NIMEIPENDA NA KWA NAMNA HII NADHANI SHENI NA TIMU YAKE WAPATIWE TENA MIAKA 5 WAMALIZIE!
ReplyDeleteNijambo la kufurahisha namatumain mazzuri kuwa angalau zita tizamwa kwa jicho la hurumi mika mingi tangu kujenga haipingu50 inafaa zijlikane mmilikiwake na karabati wake utambulike
ReplyDelete