Habari za Punde

Zanzibar ID na E- Government Yakabidhiwa Vyeti vya Ubora Utengenezaji wa Id Znz

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi na Utumishi wa Umma Ndg Abdalla Yakuot, akikabidhiwa Vyeti vya Ubora wa Utengenezaji wa Vitambulisho vya Mzanzibar kutoka kwa Mkaguzi wa Viwango vya Kimataifa ISO Mr. Amir Kahana 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi na Utumishi wa Umma Ndg Abdalla Yakuot, akikabidhiwa Vyeti vya Ubora wa Utengenezaji wa Vitambulisho vya Mzanzibar kutoka kwa Mkaguzi wa Viwango vya Kimataifa ISO Mr. Amir Kahana  kulia Mshauri Elekezi wa Usalama wa Viwango vya Kimataifa ISO Madam  Merav  Vered na kushoto Kaimu Mkurugenzi wa ZAN ID Ndg Abubakary Chilumba.

Kaimu Mkurugenzi wa ZAN ID Ndg Abubakary Chilumba akizungumza wakati wa hafla hiyo jinsi ya mafanikio ya uzalishaji wa Vitambulisho unaofanywa na Ofisi yao na kupata Vyeti vya Ubora wa huduma hiyo  na uimara wake katika hali ya kiusalama na kupata Vyeti vya Ubora vinne. Viwili vya Ubora

Vyeti Viwili  vya ubora
 IQ NET AND THE STANDARD INSTITUTION OF ISRAEL FOR QUALITY  MANAGEMENT  SYSTEM ISO. 9001

THE STANDARD INSTITUTION OF ISRAEL FOR QUALITY MANAGEMENT STANDARD  ;IS 9001

Vyeti Viwili vya Usalama
IQNET AND THE STANDARD INSTITUTION OF ISRAEL FOR INFORMATION SECURITY MANAGEMENT SYSTEM ISO 20071.

THE STANDARD INSTITUTION OF ISRAEL FOR THE INFORMATION SECURITY MANAGEMENT SERVICE ISO 27001.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kazi na Utumishi wa Umma Zanzibar, Ndg ,Abdalla Yakuot, akihutubia wakati wa hafla ya kukabidhiwa kwa Vyeti vya Ubora na Usalama wa Utengenezaji wa Vitambulisho vya Mzanzibar  kuokwa kwa Mkaguzi wa Viwango vya Kimataifa ISO . Mr. Amir Kahana, makabidhiano hayo yamefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
Wataalamu kutoka Israel, wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Ndg Abdalla Yakuot akizungumza katika hafla hiyo kulia Mkaguzi wa Viwango vya Kimataifa  ISO, Mr  Amir Kahana na Mshauri Elekezi wa Usalama wa Viwango vya Kimataifa ISO, Madam Merav Vered, wakiwa hafla hiyo.
Maofisa wa  ZAN ID wakifurahia jambo wakati wa makabidhiano hayo katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar  Ocean View Kilimani Zanzibar.
Wataalam  kutoka Israel na maofisa wa Vitambulisho wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Vitambulisho ZAN ID Ndg Abubakary Chilumbo, akizungumza katika hafla hiyo.
Mkaguzi wa Viwango vya Kimataifa ISO kutoka Israel Mr. Amir Kahana, akizungumza na kutowa maelezo ya ukaguzi wao na kuridhika kuona Ubora wa Utengenezaji wa Vitambulisho vya ZAN ID vikiwa katika kiwango cha Kimataifa na Usalama wa ubora wake.
Maofisa wa  ZAN  ID na E-Government , wakiwa katika ukumbi wa hafla ya kukabidhiwa vya Vyeti  vya Ubora wa Utengenezaji wa Vitambulisho, iliofanyika katika hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
Wafanyakazi wa ZAN ID wakiwa katika ukumbi wa hafla ya kukabidhiwa Vyeti vya Ubora wa Utengenezaji wa Vitambulisho vya Mzanzibar.

  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kazi na Utumishi wa Umma Ndg. Abdallah Yakuot , akiwa katika picha ya pamoja na Wataalum wa Viwango vya Kimataifa kutoka Israel na Maofisa wa Vitambulisho na E-Government, baada ya hafla ya kukabidhiwa Vyeti vya Ubora , hafla hiyo imefanyika katika hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.