Habari za Punde

Mafunzo ya zoezi la mezani kukabiliana na maafa yafanyika Wete

 MKURUGENZI wa Idara ya Maafa Zanzibar, Ali Juma Hamad akitoa ufafanuzi wa zoezi la Mezani la kukabiliana na maafa, kwa watendaji wa taasisi za Serikali na binafsi kwa Wilaya ya Wete huko katika Ukumbi wa Jamhuri Holi Wete.(Picha na Abdi Suleiman, Pemba)
 MKUU wa Wilaya ya Wete Mhe:Hassan Khatib Hassan, akifungua mafunzo ya siku tatu juu Zoezi la Mezani la Kukabiliana na Maafa Wilaya ya Wete, kwa watendaji wa taasisi za Serikali na Binafsi wilaya hiyo.(Picha na Abdi Suleiman, Pemba)
 WASHIRIKI wa zoezi la Mezani la Kukabiliana na maafa wilaya ya Wete, washiriki wa kundi la mawasiliano wakijadilia na mambo mbali mbali, juu la suala la maafa.(Picha na Abdi Suleiman, Pemba)
 SEKRETARI wa Idara ya Maafa kisiwani Pemba, Maimuna Faki Khamis akigawi chapisho maalumu kwa wakuu wa taasisi za Serikali na Binafsi, linaloonyesha jinsi gani ya kukabiliana na maafa yanapotokea.(Picha na Abdi Suleiman, Pemba)

 MAKAMANDA Mbali mbali wa vikosi vya ulinzi na usalama wilaya ya Wete, wakipitia kwa makini chapisho maalumu linaloonyesha jinsigani ya kukabiliana na maafa yanapotokea.(Picha na Abdi Suleiman, Pemba)
 VIONGOZI wa Taasisi za Serikali na Binafsi Wilaya ya Wete, wakipitia Chapisho maalumu linaloonyesha jinsigani ya kukabiliana na maafa yanapotokea.(Picha na Abdi Suleiman, Pemba)
AFISA mdhamini Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Pemba, Mhe:Issa Juma Ali akifunga mafunzo ya siku tatu kwa wakuu wa Taasisi za Serikali na Binafsi juu ya zoezi la Mezani la kukabiliana na maafa kwa Wlaya ya Wete.(Picha na Abdi Suleiman, Pemba)



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.