Habari za Punde

Mkutano wa taratibu za kuandika katiba na sheria watua Chakechake

MMOJA wa wananchi wa wilaya ya Chake Chake shehia ya Tibirinzi, akichangia mda juu ya taratibu za kuandikwa sheria, kwenye mkutano ulioandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, uliofanyika skuli ya Maandalizi Madungu mjini Chake Chake, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 MRATIB wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, Fatma Khamis Hemed akielezea namna ya taratibu za kuandika katiba, kwenye mkutano uliowahusishwa wananchi wa wilaya ya Chake Chake, uliofanyika skuli ya Maandalizi Madundu, kulia ni Afisa Mipango wa ZLSC tawi la Pemba, Mohamed Hassan Ali, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
SHEHA wa shehia ya Madungu wilaya ya Chake Chake Pemba, Mafunda Hamad Rubea, akifunga mkutano wa kuelimishwa wananchi wa wilaya ya Chake Chake, taratibu za kuandika sheria na katiba, kulia ni Mratibu wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, Fatma Khamis Hemed ambao ndio waandaji wa mkutano huo, uliofanyika skuli ya Maandalizi Madundu, kushoto ni wakili wa Serikali Ali Amour Makame, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.