Habari za Punde

Naibu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano, Aliambia Baraza Meli MV Mapinduzi kuwasili July2015.

Na Kijakazi Abdalla Maelezo Zanzibar

Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano imesema kuwa meli ya MV Mapinduzi 11 inatarajiwa kuwasili Zanzibar wiki ya mwisho wa mwezi julai,2015

Hayo yameelezwa na Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Mheshimiwa Juma Duni Haji wakati akiwasilisha bajeti ya Wizara hiyo 2015/2016 huko  katika Ukumbi wa Baraza la WawakilshiChukwani nje kidogo ya mji wa Zanzibar

Amesema kuwa ujenzi wa meli hiyo upo hatua za mwisho kukamilika ambapo meli inaendelea kufanyiwa vipimo na majaribio ya baharini pamoja na majaribio mengine muhimu ya vifaa na mitambo viliomo katika meli hiyo.

Aidha amesema kuwa iwapo mambo yatakwenda vizuri katika vipimo na majaribio hayo meli hiyo itaanza safari kutoka Korea ya Kusini hadi Zanzibar tarehe 25/Juni 2015 na kuwasili Zanzibar wiki ya mwisho wa mwezi Julai ,2015.

Aidha amesema kwa upande wa Shirika la Bandari linahudunia meli katika bandari za Unguja na Pemba pamoja na kusimamia usalama wa  usafiri ndani na maeneo ya bandarini


Aidha amesema kuwa shirika limehudumia jumla ya meli za kigeni 144 zenye uzito wa GRT 1,914,246, meli za ndani 2,927pamoja na vyombo vya kienyeji 3,283 pamoja na kuhudumia jumla ya tani 145,226 za mzigo mchanyiko na makontena 44,601 pamoja na mzigo wa majahazi tani 106,934.

Sambasamba na hayo Waziri huyo ameiomba Serikali liidhinishe jumla ya sh 189,108,700,000 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na maendeleo ya Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano kwa mwaka 2015/2016,ambapo Wizara itatekeleza progamu nne ikiwa ni pamoja na matumizi ya kawaida, matumizi ya kazi za maendeleo na mikopo kutoka kwa washirika wa Maendeleo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.