Na Mwanaisha Moh’d Maelezo Zanzibar
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeahidi kuwalipa walimu walioshiriki mafunzo ya kazi za amali Nchini Iran watapatiwa posho lao wanalodai na kuhakikisha wanapata haki yao ya msingi .
Hayo yameelezwa na Naibu wa Wizara Ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zahra Ali Hamad wakati akimjibu Mh Saleh Nassor Juma Jimbo La Wawi katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi huko Chukwani aliyetaka kujua ni sababu gani za msingi zinazopelekea watumishi wa Umma kunyimwa posho zao wakiwa katika safari kikazi.
Amesema serikali kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mafunzo ya Amali itahakikisha kuwa deni hilo linalipwa kwa awamu pale hali ya kifedha itakaporuhusu katika mwaka ujao wa fedha.
Amesema kutokana na uhaba wa fedha uliokabiliwa ya Mamlaka ya Mafunzo ya Amali haikuweza kuwalipa fedha hizo na badala yake kila mwalimu alilipwa dola 120 na kwa walimu 16 walilipwa jumla ya dola za Kimarekani 1920.
Amesema kuwa jumla ya Walimu 20 wakiwemo 16 kutoka vituo vitatu vya Mafunzo ya Amali watatu kutoka katika taasisi ya Karume ya Sayansi naTeknolojia na mmoja kutoka Skuli ya Sekondari ya mikunguni walihudhuria Mafunzo ya kazi za Amali Nchini Iran kwa muda wa zaidi ya mwezi mmoja.
Aidha alifahamisha kuwa wafanyakazi hao waliondoka Nchini tangu mwanzoni mwa mwaka jana kwenda nchini Iran kwa ajili ya mafunzo hayo hadi leo wanadai posho lao hilo .
“Napenda nikiri kuwa kufanyiwa malipo pungufu ilitokana na kutopatikana fedha za kutosha katika vifungu vya Mamlaka ya Mafunzo ya Amali, lakini ninakubali kuwa hilo ni deni ambalo Wizara yangu itahakikisha kuwa walimu wanalipwa haki zao hadi hivi sasa Mamlaka ya Mafunzo ya Amali ina shindwa kutekeleza kazi zake vizuri kutokana na ukosefu wa fedha”, alieleza Naibu hiyo.
Amefahamisha kuwa Mafunzo hayo yaligharamiwa na Mhisani kutoka Serikali ya Kiislamu ya Iran na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilipaswa kuwalipia posho na fedha za mavazi kwa mujibu wa taratibu za Serkali .
IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment