Na Ali Issa Maelezo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma Haruon Ali Suleiman amesema kuwa ajira Zanzibar bado ni tatizo kubwa kwa vijana kitu ambacho kinaipa changamoto Serikali kulifikiria suala hilo na kulipatia ufumbuzi na namna ya kuweza kulipunguza.
Hayo yamesemwa leo huko Mwanakwereke, Wizara ya Uwezeshaji,Ustawi wa Jamii, Vijana Wanawake na Watoto wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa Taarifa za Soko la Ajira Nchini Wizarani hapo..
Amesema Serikali imeona ipo haja kulipunguza suala la ukosefu wa ajira kwa vijana kwa kuweko mfumo wa taarifa za soko la ajira nchini ili kurahisisha mawasiliano kati ya muajiri na muajiiwa.
“Pamoja na juhudi kubwa zinazo chukuliwa na Serikali za kuimarisha Uchumi na huduma za kijamii bado hapa Zanzibar ukosefu wa Ajira kwa vijana ni tatizo,”alisema Waziri huyo.
Aidha Waziri Haruon amesema ukosefu huo wa ajira kwa nchi zinazaendelea unachangiwa na mambo mengi ikiwemo mawasiliano kati ya muajiri na muajiriwa na kukuwa kwa teknolajia za mawasiliano duniani.
Amesema hali hiyo imefanya nchi kuwa na ukosefu mkubwa wa ajira kwa raia wake kwani kazi ambazo hufanywa na watu wengi kwa sasa hufanywa mtu mmoja.
“Hivi sasa dunia imefikia pahala kupunguza waajiri kwa kurahisisha na kukua teknoloji,kwa mfano duniani sasa ukienda sheli kutia mafuta unatumia kadi tu,au ule mfumo wa posta kutuma barua watu wanatumia intaneti hivyo ile nafasi ya kumuajiri mtu kwa kazi hizi zinapitiwa”,alisema Waziri.
Hata hivyo Waziri huyo alisema ukosefu wa ajira unatokana ufinyu wa elimu na ujuzi wa kitaalamu jambo ambalo linapelekea vijana wegi kukosa sifa katika ajira.
Nae Mkurugenzi wa ajira Ameir Ali Ameir alisema katika mwaka 2009 Serikali ya Zanzibar kupitia Wizara ya Kazi Maendeleo ya Vijana Wanawake na Watoto wakati wanaandaa Sera ya ajira na lengo kuu la sera hiyo ni kuongeza tija na kupata ajira zenye heshima, faida na zilizo chaguliwa kwa hiari ili kupunguza ukosefu wa ajira.
Amesema Ufunguzi wa Mfumo niwenye manufaa kwa wananchi hasa wa Zanzibar ambao umeekewa website yake hivyo utakuwa rahisi kufuatilia ajira bila ya usumbufu.
Mkurugenzi huyo aliwaomba wandishi wa habari kuutangaza ufumo huo mjini na vijijini ili kuweza kuenea na kupata taarifa hizo kwa jamii.
No comments:
Post a Comment