Habari za Punde

Askari wa Usalama barabarani wapatiwa mafunzo ya haki za binadamu Chakechake

 ASKARI Polisi wa usalama barabarani wa mikoa miwili ya Pemba, wakimsikiliza Mratibu wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, Fatma Khamis Hemed, wakati akielezea namna ZLSC inavyofanyakazi zake kwa kuisadia jamii, kwenye mafunzo ya haki za binadamu kwa askari hao yaliofanyika kituo cha sheria Chake Chake Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 ASKARI Polisi wa usalama barabarani wa mikoa miwili ya Pemba, wakiwa wamesimama kuimba wimbo wa maadili, kabla ya kuanza kwa mafunzo ya haki za binadamu, yalioandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, yaliofanyika kituoni hapo mjini Chake Chake Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 MKUU wa usalama barabarani mkoa wa kusini Pemba, Shawal Abdalla Ali, akifungua mafunzo ya haki za binadamu kwa askari wa usalama wa barabarani wa miko miwili ya Pemba, yalioandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, na kufanyika Kituoni hapo mjini Chake chake, kulia na Afisa Mipango wa kituo hicho Siti Habibu Mohamed na katikati ni Mratibu wake, Fatma Khamis Hemed, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
 MRATIBU wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, Fatma Khamis Hemed, akisiliza jawabu alilomuliza mshiriki wa mafunzo ya haki za binadamu, askari polisi, ‘maana na katiba ya nchi’ ambapoa alijibu vizuri, kwenye mafunzo hayo yaliondaliwa na ZLSC, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
AFISA Mipango wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC, tawi la Pemba Siti Habibu Mohamed, akitoa mada juu ya haki za binadamu, kwa askari polisi wa usalama barabarani wa mikoa miwili ya Pemba, mafunzo yaliofanyika Kituo cha huduma za sheria Chake chake Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.