Habari za Punde

Yaliojiri Bonaza la Masauni Cup Mchezo wa Fainali Mkunazini na Miembeni Viwanja vya Mnazi Mmoja Mkunazini Imeshinda 1--0

Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Hamad Masauni akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi kwa Washindi wa Bonaza la Masauni Cup,lililoandaliwa na Mbunge huyu kuwakutanisha vijana na kukuza vipaji vya mchezo wa Soka Zanzibar kuirudisha Zanzibar katika medali yake ya Soka enzi hizo, Bonaza hilo limeandaliwa na Mbunge huo Masauni.
Waziri Kiongozi Mstaaf wa Zanzibar Mwakilishi wa Mwanakwerekwe Zanzibar Mhe Shamsi Vuai Nahodha, akitowa nasaha zake kwa Vijana wakati wa michezo ya Bonaza ya Kombe la Masauni Cup Vijana ndio taifa la kesho inabidi kudumisha amani kupitia katika michezo na michezo ni ajira kwa Vijana  
Wapenzi wa mchezo wa Soka Zanzibar wakifuatilia mchezo huo wa fainali ya Bonaza la Masauni Cup, katika viwanja vya mnazi mmoja lililokuwa likifanyika usiku.
Machoka wa Timu ya Mkunazini waliofanikisha timu yao kutoka na Ubingwa wa Kombe la Bonaza la Masauni Cup wakiwa katika uwanja huo wakati wa mchezo wao wa fainali na timu ya Miembeni
Kipa Bora wa michuano ya Kombe la Bonaza Masauni Cup Abui akizungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo wao wa fainali na timu ya miembeni kumalizika kwa ushindi wa bao 1--0 
Wachezaji wa timu yac Mkunazini na Miembeni wakipongezana baada ya mchezo kumalizika michezo ni udugu na urafiki.

Waziri Kiongozi Mstaaf Mwakilishi wa Jimbo la Mwanakwerekwe Mhe Shamsi Vuai Nahodha akiwa na kitita cha fedha za mshindi wa Pili wa Bonaza la Masauni Cup, Mshindi wa Pili timu ya Miembeni imekabidhiwa shilingi Laki Tano kwa kushika nafasi ya Pili ya Bonaza hilo.
Waziri Kiongozi Mstaaf wa Zanzibar Mwakilishi wa Jimbo la Mwanakwerekwe Zanzibar Mhe Shamsi Vuai Nahodha akimkabidhi zawadi mshindi wa Pili wa Bonaza la Masauni Cup kitita cha shilingi Laki Tano kwa kushika nafasi ya Pili ya Bonaza hilo.Baada ya kufungwa bao moja na timu ya Mkunazini.katika mchezo wa Fainali uliofanyika katika viwanja vya malindi Zanzibar
Mhe Shamsi Vuai Nahodha na Mbunge wa Kikwajuni Mhe Eng Hamad Masauni wakisalimiana na wachezaji wa timu ya Mkunazini Mabingwa wa Bonaza a Masauni Cup baada ya kuifunga timu ya Miembeni katika mchezo wa fainali ya Bonaza la Masauni Cup uliofanyika katika viwanja vya malindi mnazi mmoja, Bonaza hilo ni kwa ajili ya kuninua vipaji vya Vijana katika mchezo wa Soka Zanzibar.
Waziri Kiongozi Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mwakilishi wa Jimbo la Mwanakwerekwe Mhe Shamisi Vuai Nahodha, akimkabidhi Kombe la Ubingwa wa Bonaza la Masauni Cup Nahodha wa Timu ya Mkunazini Abui baada timu yao kuifunga timu ya Miembeni katika mchezo wa fainali uliofanyika uwanja wa malindi mnazi mmojaTimu hiyo imeshinda bao 1--0. kulia Mbunge wa Kikwajuni Mhe Eng Hamad Masauni. Bingwa wa Bonaza hilo amekabidhiwa Fedha Tasilim shilingi milioni moja na Kikombe.
Kipa Bora wa Michuano ya Bonaza la Masauni Cup na nahodha wa timu ya Mkunazini Abaui akiwa na Kombe la Ubingwa wa Bozana na fedha taslim shilingi milioni moja zimekabidhiwa kwa timu Bingwa wa Bonaza hilo lililofadhiliwa na Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar Mhe Eng Hamad Masauni, lililozishirikisha timu za Vijana za Majimbo kuinua Vijana vya mchezo wa Soka Zanzibar, 

Kikosi cha Timu ya Mkunazini wakisherehekea Ubingwa wao wa Bonaza la Masauni Cup baada ya kuibuka mshindi kwa kuifunga timu ya Miembeni kwa bao 1--0. mchezo uliofanyika katika viwanja vya malindi Mnazi Mmoja Zanzibar.
Wapenzi wa tim u ya Mkunazi wakiwa na Kombe lao la Bonaza la Masauni Cup wakipiga picha ya kumbukumbu baada ya mchezo wao wa fainali. 
Wapenzi wa timu ya Mkunazini wakisherehekea ushindi wa timu yao wakati wa mchezo wa fainali dhidi ya timu ya Miembeni kwa ushindi wa bao 1--0.Mchezo uliofanyika katika viwanja vya Malindi Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.