Habari za Punde

Mama Mwanamwema Awatembelea Watoto wa Kijiji cha SOS na Nyumba ya Watoto Mazizini Unguja Kutoa Mkono wa Eid Fitr.

Watoto wa Kijiji cha SOS wakimpokea Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, alipofika katika makaazi yao kuwatembelea na kutoa mkono wa Eid Fitry kwa watoto hao, Kijijin cha Watoto SOS kilichoko mombasa Zanzibar. 
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na Viongozi wa Kijiji cha Watoto SOS, baada ya kuwasili katika kijiji hicho kuwatembelea Watoto hao na kutoa mkono wa Eid Fitry.
Mkurugenzi Mipango wa Kijiji cha SOS, akitowa maelezo kwa Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema alipofika kuwatembelea Watoto hao na kutowa mkono wa Eid Fitry. 
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akitowa mkono wa Eid kwa watoto wa kijiji cha SOS akiwa na Mgombea Mweza Mhe Samiha Suluhuhu Hassan akijumuika na Mama Shein.
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akimpa mkono wa Eid Mtoto mtoto anayeishi katika kijiji cha watoto cha SOS mombasa Zanzibar alipofika kutoa mkono wa Eid kwa watoto hao.
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akisalimiana na Walezi wa Nyumba ya Watoto Yatima Mazizini Zanzibar baada ya kuwasili katika nyumba hiyo kuwatemblea Watoto hao na kutoa Mkono wa Eid Fitry.
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akiwasalimia Watoto wa Nyumba ya Watoto Yatima Mazizini wakati alipofika kuwatembelea na kutoa mkono wa Eid Fitry.  
Watoto wa Nyumba ya Watoto Yatima Mazizini Zanzibar wakimsikiliza Mama Mwanamwema Shein, wakati alipofika kuwatembelea na kuwapa mkono wa Eid Fitry.
Mama Mwanamwema Shein akitowa mkono wa Eid Fitry kwa watoto wa Nyumba ya Watoto Yatima Mazizini Zanzibar akiwa na Mgombea Mweza wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samiha Hassan Suluhu.
Mtoto Faidhuni Joseph akisoma dua baada ya kumalizika kwa maongezi na Mama Mwanamwema Shein, alipofika katika makaazi yao kuwatembelea na kutoa mkono wa Eid Fitry.  
                       Mama Mwanamwema Shein, na Waziri Mhe Bizaina Omar wakiitikia dua

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.