Habari za Punde

Kampeni ya Kinyanganyiro cha Kuwania Ubunge na Uwakilishi Jimbo la Chumbuni Kimeanza leo Tawi la Chumbuni

Wagombea Udiwani Ubunge na Uwakilishi wakiwasili katika Tawi la CCM Chumbuni kwa ajili ya kuaza kampeni ya kuomba kura kwa Wananchi wa Tawi hilo ikiwa ni mkutano wa uzinduzi uliofanyika leo asubuhi tawini hapo
Wananchi wa Tawi la Chumbuni wakishangilia kwa Wimbo wa CCM CCM CCM wakiwasili wagombea hao tayari kwa uzinduzi wa Kampeni Tawi hapo.
Wagombea Ubunge Uwakilishi na Udiwani wakiwa katika Tawi la CCM Chumbuni tayari kwa kujieleza kwa Wananchi wa tawi hilo kuomba kura katika uchaguzu utakaofanyika tarehe 1-8-2015
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Chumbuni Ndg Ahmada Suleiman Hassan akitowa maelezo kwa Wagombea mambo ya kuzingatia wakati wa kujieleza na kutoa taarifa kwa Wananchi utaratibu wa mkutano huo usiwe wa kushangilia kwa mgombea ajilieleza , Kila Mgombea amepewa dakika tano za kujieleza kwa wananchi.
Msimamizi wa Uchanguzi akitowa maelekezo kwa mgombea Ubunge wa Jimbo la Chumbuni Ussi Salum Pondeza HAMJAD, kabla ya kuza kujieleza na kuomba kura kwa Wananchi wa Tawi hilo la Chumbuni Jimbo la Chumbuni Zanzibar.
Mgombea Ubunge Jimbo la Chumbuni Ndg Ussi Sulam Pondeza akijieleza kwa Wananchi wakati wa uzinduzi wa kampeni uliofanyika katika tawi la CCM Chumbuni leo asubuhi.ukiwa ni mkutano wa mwazo jimboni hapo
Mgombea Ubunge Jimbo la Chumbuni akijibu sawala aliloulizwa kuhusiana na fedha za Jimbo atazitimia vipi? na kujibu fedha hizo zitatumika katika jimbo hilo kwa maendeleo ya jimbo na wananchi wake.
           Wananchi wa Tawi la CCM chumbuni wakifuatilia mkutano wa kampeni tawini hapo.
Mgombea nafasi ya Udiwani Wadi ya Chumbuni Ndg Juma Ngwali Juma akijieleza na kuomba ridhaa za wananchi wa tawi hilo kumchagua kwa mara ya Pili baada ya kumaliza kipindi chake 
Mgombea Udiwani Ndg Mussa Haji Idrisa akijinadi kwa Wananchi wa Tawi la Chumbuni kuomba kura wakati wa mkutano wa kampeni. uliofanyika Tawi la Chumbuni 
Ndg Khamis Ali Mohammed akijitokeza kugombea Udiwani Wadi ya Chumbuni akiomba kura kwa wananchi.
Mgombea Nafasi ya Uwakilishi Jimbo la Chumbuni N dg Hafidh Haji Faki akijinadi kwa Wananchi wa Jimbo la Chumbuni kuomba ridhaa zao wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika tawani hapo ukiwa ni mkutano wa uzinduzi
Wananchi wa Tawi la Chumbuni wakifuatiliwa wagombea wao walipokuwa wakijieleza kuomba kura.
Mgombea nafasi ya Uwakilishi Ndg Khamis Omar Seif, akiomba kura kwa Wananchi wa jimbo hilo wakati akijieleza
Mgombea nafasi ya Uwakilishi Ndg Miraj Khamis Mussa akitoa sera zake kwa wananchi wa tawi la CCM Chumbuni wakati wa mkutano wake wa kampeni tawini hapo na kutoa ahadi kwa wananchi hao.
Mbunge wa zamani wa Jimbo la Chumbuni Mhe Perera Ame Silima akitetea kiti chake cha Ubunge wakati wa mkutano wa kampeni katika tawi la CCM chumbuni 
Mwalimu Shabab Salum Jabir, akitowa sera zake kwa vijana wakati wa mkutano wake wa kampeni


2 comments:

  1. hawa akina Amjad wamesoma? sio anakwenda kwenye bunge mtu mbumbumbu kuwakilisha Zanzibar, matokeo yake wanatuadhirisha tunaonekana Zanzibar wote hawana maana, naona sasa imekuwa kila mtu anautaka ubunge mpaka yule mtoto wa Comandoo, tuwekeeni CV zao kwanza tujuwe wao ni akina nani, CCM isiwe chaka la watoro ndio maana hatuendelei

    ReplyDelete
  2. mdau hapo juuu nimekuelewa sanaaaaa yako uko sahihi

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.