Habari za Punde

CAG aongoza kikao cha bodi ya wakaguzi ya UN

  Wajumbe wa  Bodi ya Ukaguzi kutoka kushoto, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa  Serikali ya India,  Bw. Shashi Kant Sharma,  Sir Amyas Morse,  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu kutoka Serikali ya India na Bw. Mussa Juma Assad,  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu kutoka Serikali ya Tanzania wakitia saini zao katika  ripoti 28 za ukaguzi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa zilizorejewa na kupitishwa na Bodi hiyo wakati wa mkutano wake wa siku mbili. ripoti hizo ni  matokeo ya kazi kubwa ya Bodi hiyo

 Mdhibiti na  Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na ambaye pia ni Mwenyekiti wa  Bodi ya  Ukaguzi ya  Umoja wa  Mataifa, Bw.Mussa Juma Assad akizungumza wakati wa hitimisho la mkutano wa siku mbili wa Bodi hiyo uliofanyika hapa Umoja wa Mataifa kuanzia Julai 22-23. Kushoto kwake ni Bw. Fransis Kitauli,  Mkurugenzi wa Ukauzi wa Nje  na  Mwenyekiti wa  Kamati ya  Operesheni za Ukaguzi ( AOC) Akiwa Mwenyekiti wa   AOC Bw. Kitauli ambaye alishika nafasi  hiyo tangu mwaka 2012 amefanikisha  utoaji wa ripoti za ukaguzi za Umoja wa Mataifa kwa  miaka mitatu mfululizo


Ujumbe wa Bodi ya Tanzania ambao ni  kutoka kushoto Jerome Francis, Naibu Mkurugenzi ukaguzi wa Nje,  Bw. Salhina Mkumba,  Naibu Mkurugenzi, Ukaguzi wa Nje na ambaye amefanya kazi kwa karibu sana  na  Bw. Fransis Kitauli tangu Ofisi ya  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali  ilipoteuliwa kuingia kwenye Bodi ya Ukaguzi ya  Umoja wa Mataifa wa mwisho ni  Bw.  Athuman S. Mbuttuka, Naibu Mkaguzi Mkuu.

Na Mwandishi Maalum,   New York

          Bodi ya  Ukaguzi wa Hesabu za     Mashirika ya Umoja wa Mataifa ,  imemaliza mkutano wake wa siku mbili kwa  kurejea na kupitisha taarifa 28  za ukaguzi.

Taarifa  22 kati ya hizo zitawasilishwa mbele ya   Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na  sita zitawasilishwa  kwa  Mamlaka na vyombo vingine.

Mkutano huo  umefanyika   hapa  Umoja wa  Mataifa  chini ya Uenyekiti wa  Mkaguzi na Mdhibiti  Mkuu wa  Hesabu za Serikali kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bw. Mussa Juma Assad

Wajumbe wengine wa Bodi ni    Mdhibiti na  Mkaguzi Mkuu kutoka Serikali ya Uingereza  Sir Amyas Morse na  Bw. Shashi Kant Sharma,  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu kutoka  Serikali ya  India.

Akizungumza  mara baada ya kutia saini  taarifa hizo,  jukumu lililofanywa kwa  pamoja  na  wadhibiti na  Wakaguzi hao watatu,  Bw. Mussa Juma Assad amewashukuru  wajumbe wenzie kwa  kazi kubwa na nzuri   ambayo wameifanya katika siku  hizo mbili pamoja na  ushirikiano mzuri waliompatia.
“  

Nichukue fursa hii kuwashukuru sana kwa  kazi hii nzuri na ushirikiano mkubwa mlionipatia,  ushirikiano ambao umetuwezesha kukamilisha kazi hii kwa wakati na muda muafaka”, akasema  Mdhibiti  na Mkaguzi  Mkuu wa  Hesabu za serikali   Bw. Assad

Wakijibu   shukrani hizo,  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu kutoka Serikali ya  Uingereza, Sir  Amyas Morse  alimshukuru Mwenyekiti  kwa uongozi wake na upeo mkubwa ikiwa ni pamoja na  ushirikiano wake  kwa  wajumbe wenzie.

 Akatumia pia fursa hiyo kumpongeza na kumshukuru  kwa moyo wa dhati,  Bw. Fransis Kitauli ambaye  kwa  miaka  mitatu akiwa  Mwenyekiti wa  Kamati ya Operesheni amefanikiwa kutolewa kwa  ripoti za ukaguzi bila kukosa.

Sir Morse amemuelezea Bw. Kitauli kama Mkurungezi na  Mwenyekiti ambaye ameonyesha weledi  mkubwa na  kujituma kwa hali ya juu  katika utekelezaji wa majukumu yake  amekuwa  Mkurugenzi anayemwakilisha Mkaguzi  Mkuu hapa Umoja wa Mataifa  kwa uadilifu wake, na weledi  mkubwa katika utekelezaji na usimamizi wa majukumu yake  na akamtakia kila la kheri arejeapo  Tanzania. 

Kwa  upande wake   Mkaguzi  na Mdhibiti Mkuu  wa Serikali ya  India, Bw. Shashi Sharma, pamoja na kumshukuru Mwenyekiti kwa  uongozi wake mahili naye alimpongeza  na kumshukuru   Bw. Fransis Kitauli kwa uhodari wake,  kujituma  na   kazi kubwa aliyoifanyia katika   utekelezaji na usimamizi  wa majukumu  ya  Bodi hiyo.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.