Habari za Punde

MAOFISA UCHAGUZI WA TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI TANZANIA WAPIGWA MSASA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU.


Na.Abdi Suleiman.
Waratibu na wasimamizi wa Uchaguzi na wasimamizi wa wasaidizi ngazi ya jimbo wametakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria , katiba, kanuni na miongozo  ya Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi ili kuepusha kuwa chanzo cha migogoro inayotokana na Uchaguzi.

Hayo  yalielezwa na Makamo Mwenyekiti wa Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania, Jaji mstaafu wa Mahakama ya Rufaa Tanzania Mbarouk Salim Mbarouk huko katika ukumbi wa kiwanda cha Mafuta ya Makonyo Wawi Kisiwani Pemba alipokuwa akifunguwa mafunzo kwa watendaji hao.

Alisema uteuzi wao umezingatia sheria za Uchaguzi kifungu namba 6 (1)  na kifungu cha 8 na(1) na (2) cha sheria ya Uchaguzi wa Rais . Wabunge na Mdiwani namba 1 ya mwaka 2024.

Alieleza hivo watendaji hao  wanawajibu wa kusimamia na kuratibu shughuli za Uchaguzi kwa uadilifu , uaminifu, Uzalendo  uchapazi uliotukuka.

Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa Tanzania na Makomo Mwenyekiti wa Tume huru ya Uchaguzi Tanzania, Mbarouk Salim Mbarouk alisema ni vyema kwa watendaji hao kuzingatia masharti ya Ibara ya 74(6)  YA Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kwa Tume huru ya Uchaguzi ndio yenye  jukumu la kusimamia , kuratibu uendeshaji wa uchaguzi wa Rais na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano na Madiwani kwa Tanzania bara.

Alifahamisha kuwa dhamana waliopewa watendaji hao ya kusimamia na kuratibu uendeshaji wa Uchaguzi wa Rais na wabunge wa Jamhuri ya Muungano ni kubwa , nyeti na muhimu kwa mustkbali wa Taifa la Tanzania.

‘’Fanyeni kazi zenu kwa misingi ya kisheria na uadilifu kwani dhamana mulipewa ni kubwa hivyo itendeeni haki kwani Tume huru ya Uchaguzi inawategemeeni kwa kuzingatia utendaji wenu katika kipindi chote cha utumishi wenu hadi hapo mutakapokamilisha jukumu hili la uchaguzi mkuu’’, alisema.

Alisema Uchaguzi ni mchakato unaojumuisha  hatuwa na taratibu mbali mbali za kikatiba na kisheriaambazo hupaswa kufuatwa na kuzingatiwa kwani ndio msingi wa Uchaguzi kuwa mzuri na wenye ufanisi na hivyo kupunguza kama sio kuondosha kabisa malalamiko au vurugu wakati wote wa mchakato wa Uchaguzi.

‘Pamoja na uzoefu ambao baadhi yenu munao katika kuendeshea uchaguzi , msiache kusoma katiba , Sheria, kanuni , miongozo na fuateni n atekelezeni maelekezo mbali mbali yatokayokuwa yanatolewa na Tume’’, alisema.

Aliwataka watendaji hao kuvishirikisha vyama vyote vya siasa vyenye usajili kamili katika hatua zote kwa kuzingatia matakwa ya katiba , sharia na kanuni na maelekezo mbali mbali ya Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi sambamba na kuwashirikisha wadau wa Uchaguzi hususan katika maeneo ambayo kwamujibu wa katiba , Sheria , kanuni, miongozo na maelekezo mbalimbali yaliotolewa na yatakayotolewa na Tume ambayo wanastahili kushirikishwa.

‘’Ajira za Watendaji wa Vituo zingatieni kuajiri watendajiwenye weledi, wanaojitambuwa, Wazalendo, waadilifu na wacahapakazi na kuachana na upendeleo kwa ndugu na jamaa ambao hawana sifa za kufanyashuhuli za Uchaguzi’’, alifahamisha.

Alisema ni vyema wakati wa kuapisha mawakala , wakatoa taarifa mapema kwa vyama vya siasa kwa mujibu wa sharia, kanuni na maelekezo ya Tume , kuvipatia vyama vya siasa orodha ya vituo vya kupigia kura ili kuviwezesha kupanga mawakala.

Alifahamisha kuwa kifungu cha 20 cha sharia ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi namba 2 ya mwaka 2024 kinasema. Mtumishi alieajiriwa , alieteuliwa au aliyeazimwa na Tume, kwa kipindi chote atakachokuwa anatekeleza majukumu ya Tume atachukuliwa kuwa ni Mtumishi wa Tume.

Hivyo watatakiwa kuzingatia katiba, Sheria hiyo , sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani na sheria nyengine  yoyote inayohusu utekelezaji wa majukumu ya Tume,hivyo wote ni watumishi wa tume Huru ya Tifa ya Uchaguzi katika utekelezaji wa majukumu yao ya Uchaguzi.

Alifahamisha kuwa utendaji na uwajibikaji wao katika kipindi chote cha utumishi kwa Tume , watawajibika Kwa Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi na sio mamlaka nyengine , ispokuwa kama kuna jambo linahitajika kwa mujibu wa sheria nengine za nchi na kwamba taarifa zozote za Uchaguzi zinapaswa kutolewa kwa Tume na sio vyenginevyo ama kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Uchaguzi.

Jaji Mbarouk aliwataka watendaji hao kutunza na kusimamia viapo vyao kwa kutunza siri na kujitowa au kutokuwa wanachama wa chama cha siasa katika kipindi chote cha Uchaguzi, sambamba na kuzingatia mafunzo waliopewa na kutowa uzoefu wao wa usimamizi wa siku za nyuma.

Kwa upande wake Hakimu wa Mahakama ya mwanzo Chake Chake Nassor Suleiman Nassor baada ya kuwalisha viapoa aliwasihi watendaji hao wa Uchaguzi wa Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi kutokuwa Chanzo cha uvunjifu wa Amani na wafanyekazi kwa uadilifu ili kuondowa malalamiko yasiokuwa ya lazima kwa wadau wa Uchaguzi.

Alisema kuwa nafasi waliopewa ni nyeti kutokana na umuhimu na ukubwa wake hivyo wafanye kazi ipasavyo kwa kuitumikia vyema hiyo kwani Taifa lote linawangalia wao.

Hata hivyo kaimu mkurugenzi Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar, Adama Mkina alisema mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo maofisa mbali mbali wa Uchaguzi ili waweze kufanya kazi hiyo kwa mujibu wa Sheria na katiba ya nchi ili Uchaguzi huo uwe huru na haki.




No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.