Habari za Punde

Wacomoro sita waliookotwa Pemba warejeshwa kwao


Na Haji Nassor, Pemba                                    
WALE watu sita waliodhaniwa kuwa ni wavuvi raia wa visiwa vya Comoro, ambao waliokotwa wiki iliopita bahari ya Matumbilini wilaya ya Mkoani Pemba, baada ya kupotea tokea Mei 11 mwaka huu, tayari ofisi ya wilaya ya Mkoani imeanza tataribu za kuwarejesha kwao.
Mkuu wa wilaya hiyo Hemed Suleiman Abdalla, aliliambia gazeti hili kuwa, juzi watu hao walishasafirishwa na uongozi wa wilaya yake kwa meli ya M.V Serengeti hadi Unguja.
Alisema uongozi wa wilaya, uliwasafirisha watu hao wakiongozana na afisa mmoja kutoka Idara ya Uhamiaji pamoja na askari Polisi wa bandarini (Police marine) kwa ajili ya kumaliza tataratibu zao na kisha kukabidhiwa kwa ubalozi wa nchi yao uliopo Zanzibar.
Alieleza kuwa baada ya kujirdhisha, ndio hapo juzi walifikia uamuzi kwamba watu wao wafikishwe kwenye ubalozi mdogo wa nchi yao, ambapo nao utafanya tataribu za kinchi kwa ajili ya kuwafikisha Comoro ili wakutane na falimia zao.
“Kwa kweli sisi kama uongozi wa wilaya ya kwa kushirikiana na taasisi nyengine za kisheria, tumeshawasafirisha wale watu sita raia wa Comoro, ingawa kwanza watafikia Unguja kwa taratibu nyengine’’,alifafanua.

Aidha Mkuu huyo wa wilaya ya Mkoani, amezipongeza taasisi mbali mbali wilayani mwake, kutokana na kuonyesha ushirikiano wa dhati tokea Juni 24, walipookotwa watu hao kwenye bahari ya Matubilini na kisha kufikishwa hospitali wa matibabu.
Watu hao ambao walijitambaulisha kuwa ni wavuvi ni nahoza Alloui Huomad Mromaji (40), msaidizi nahoza Yunus Maishe Mussa (45), Deiyan Ahamad Wali (25), Hassan Mmadi Abdul (59), Ibrahim Mzee Said (45) na Abdalla Abdurr-ahaman Abass (35) wote wakaazi wa visiwa vya Comoro.
Watu hao waliodhaniwa kuwa ni wavuvi, walisema walipotea tokea Mei 11 mwaka huu, wakati wakitoka kiswa cha Mayotte kununu chakula, na kwenda Anzuwani, amapo baada ya kuishiwa na mafuta na chombo chao aina ya ‘Fiber’ walibururuwa na upepo hadi kuokotwa Pemba Juni 24 mwka huu.

Hii ni mara ya pili ndani ya mwaka huu kwa wavuvi kutoka Comoro kuokotwa bahari ya Mkoani kwa madai ya kubururwa na upepo ambapo mwezi uliopita waliokotwa wavuvi wawili.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.