Mgombea Urais kupitia Chama cha DP Ndg. Abdallah Kombo Khamis akiwa na Viongozin wa Chama hicho wakifuatilia maelezo yakisomwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mhe Jecha S Jecha akimkabidhi mkoba ukiwa nas Fomu za kugombea Urais wa Zanzibar Mgombea Urais wa Chama cha DP Ndg Abdallah Kombo Khamis, hafla hiyo imefanyika katika Afisi za Tume za Uchaguzi Hoteli ya Bwawani Zanzibar.
Mgombea Urauis kupitia Chama cha DP Ndg. Abdallah Kombo Khamis akionesha mkoba wake ukiwa na Fomu za kugombea Urais wa Zanzibar baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mhe Jecha S Jecha katika Afisi za Tume ya Uchaguzi zilioko hoteli ya Bwawani Zanzibar.
Mgombeav Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Democratic Party ( DP ) Ndg Abdallah Kombo Khamis akiwa na Wanachama wake baada ya kukabidhiwa Fomu ya kuwania Urais wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba 2015. wakiwa katika ukumbi wa Salama Bwawani baada ya kukabidhiwa fomu hizo.
No comments:
Post a Comment