SPIKA wa Baraza la Wawakilishi, Zanzibar Mhe. Pandu Ameir Kificho akiwa katika mazungumzo na Viongozi wa Jumuiya ya nchi za Ulaya ( EU) hapo Baraza la Wawakilishi Chukwani
SPIKA wa Baraza la Wawakilishi, Zanzibar Mhe. Pandu Ameir Kificho akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Jumuiya ya nchi za Ulaya ( EU) hapo Baraza la Wawakilishi Chukwani
Na, Himid
Choko BLW.
SPIKA wa Baraza la Wawakilishi, Zanzibar Mhe. Pandu Ameir Kificho ameelezea matumaini yake kwamba uchaguzi ujao utakuwa huru na wa haki.
Amesema hali
hiyo itachangia kwa kiasi kikubwa kuendelea
kuwepo kwa hali ya amani na utulivu
hapa nchini suala ambalo ni muhimu kwa
mustakbali wa maendeleo ya taifa na
ustawi wa jamii.
Spika
Kificho amesema hayo leo, huko Afisini kwake
Chukwani wakati akizungumza na
Viongozi wa Jumuiya ya nchi za Ulaya ( EU) waliongozwa na Balozi wa Umoja huo hapa
nchini Bwa Filiberto Sebregondi.
Kificho ameufahamisha ujumbe huo kwamba, ameridhishwa na ahadi zinazotolewa na wadau
wote wa uchaguzi ikiwemo Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Viongozi wa vyama
vya Siasa na vyombo vya Ulinzi na Usalama kwamba kila kimoja kitatekeleza vyema
wajibu wake ili kufanikisha uchaguzi huo
kwa njia ya haki, amani na usalama.
“Kila
taasisi, tayari imetuhakikishia kwamba itatekeleza wajibu wake na kuondosha
vikwazo vyote kwa lengo la kuendesha
salama mchakato wote wa Uchaguzi ambao tunaamini utakuwa wa haki na
utulivu mkubwa” alisisitiza Spika Kificho.
Aidha spika
Kificho ameuhakikishia umoja huo kwamba
Serikali zote mbili zitafanya kila liwezalo kuhakikisha kwamba hali ya
amani na usalama inaendelea kuwepo
wakati na baada ya uchaguzi .
Kuhusu
Serikali ya Umoja wa Kitaifa Spika kificho amesema mfumo huo ambao umekubaliwa
na wananchi wenyewe upo kikatiba hivyo Baraza la Wawakilishi litafanya kila
liwezavyo kulinda matakwa hayo ya wananchi.
Amesema
chini ya mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambao ni adimu duniani,
maendeleo makubwa ya kisiasa na kiuchimi
yamepatikana na umoja wa wananchi
unazidi kuimarika hapa Zanzibar.
Amesema Baraza la Wawakilishi la Nane linalomaliza
muda wake lilikua la aina yake ambapo chini ya mfumo wa Serikali ya Umoja wa
Kitaifa Wajumbe wasiokua Mawaziri
waliibana vyema serikali kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji , suala
ambalo lilitoa mvuto mkubwa kwa wananchi kufuatilia mikutano ya Baraza hilo.
Nae
Balozi Filiberto Sebregondi amewaomba wadao wote wa uchaguzi kufuata
sheria na taratibu zote ili kufanikisha
vyema mchakato wote wa uchaguzi huru na
wa haki.
Amesema
jumuiya ya ulaya kwa kiasi kikubwa inafuatilia
mchakato huo na kuwatakia kila la
kheri wananchi na hatimae waweze kufuka
salama katika uchaguzi huu.
Mwisho.
Imetolewa na
Himid
Choko
Afisi ya Baraza la Wawakilishi, Zanziabar,
25 August 2015
No comments:
Post a Comment