Habari za Punde

Waandishi Zanzibar wapatiwa mbinu bora kuripoti habari za Uchaguzi

 Afisa Mwandamizi Baraza la Habari Tanzania Ofisi ya Zanzibar Shifaa Said Hassan (aliesimama)  akifahamisha kitu katika mafunzo ya siku tano yalimaliza jana Agosti 28 yaliyoandaliwa na Shirika  la Habari la Marekani  Internews  kwa waandishi wa Habari wa Zanzibar katika Ukumbi wa Umoja wa watu wenye Ulemavu Kikwajuni Mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

 Mwandishi Mkongwe wa Tasnia ya Habari Tanzania ambae pia ni Mkurugenzi wa Internews Tanzania Valerie N. Msoka akifafanua kitu kwa wandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo juu ya kuripoti uchaguzi Mkuu.
 Badhi ya waandishi wa habari walioshiriki mafunzo juu ya kuripoti Habari za Uchaguzi Mkuu wakisikiliza nasaha zilizotolewa na Mkurugenzi wa Internews Tanzania Valerie N. Msoka (hayupo pichani) katika mafunzo yaliofanyika Ukumbi wa Umoja wa watu wenye ulemavu Kikwajuni Mjini Zanzibar.

 Mkurugenzi wa Shirika la Internews kanda ya Afrika Ian Noble akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari juu ya kuripoti habari za Uchaguzi, alipotembelea katika mafunzo hayo huko ukumbi wa watu wenye ulemavu Kikwajuni Weles Mjini Zanzibar.


Mkurugenzi wa Shirika la Internews kanda ya Afrika Ian Noble (wakatikati) katika picha ya pamoja na washiriki na wasimamizi wa mafunzo hayo (kulia) aliekaa ni Afisa Mwandamizi Baraza la Habari Tanzania Ofisi ya Zanzibar Shifaa Said Hassan na kushoto ni Mwandishi Mkongwe wa Tasnia ya Habari Zanzibar Salim Said Salim.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.