Habari za Punde

Mkurugenzi wa Kinga na elimu ya afya atoa tahadhari juu ya ugonjwa wa kipindupindu


Mkurugenzi Kinga na elimu ya afya Dkt. Mohd Dahoma akizungumza na waandishi wa Habari  Ofisini kwake Wizara ya Afya juu tahadhari ya ukonjwa wa Kipindupindu hivyo amewashauri wananchi kununua chakula kilicho hifadhiwa vizuri ama chakula kimoto na kujiepusha kutumia juice zinazotengenezwa kienyeji. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar        

Wananchi wametakiwa kuchukua tahadhari ya  vyakula na vinywaji  katika viwanja vya sikuu inayoanza kesho kutokana na tishio la maradhi ya kuharisha na kutapika ambayo yameanza kujitokeza  katika nchi jirani.

Akizungumza na waandishi wa Habari  Ofisini kwake Wizara ya Afya, Mnazimmoja, Mkurugenzi Kinga na elimu ya afya  Dkt. Mohd Dahoma amewashauri wananchi kununua chakula kilicho hifadhiwa vizuri ama chakula kimoto na kujiepusha kutumia juice zinazotengenezwa kienyeji.

Dkt. Dahoma amesema katika viwanja vya  sikukuu kunakuwa na mkusanyiko mkubwa wa watu na biashara ya vyakula na vinywaji vinakuwa vingi hivyo ameshauri watu wawe waangalifu chakula cha kununua.

“Chakula baridi na Juice zilizotengenezwa kwa njia za kienyeji sio busara kuzitumia katika kipindi hiki kwani hakuna uhakika wa maji yaliyotumiwa kutengeneza bidhaa hizo.”alisisitiza Dkt Dahoma.


Amewashauri wananchi kuwasimamia watoto wao wanapotaka kununua chakula katika viwanja vya sikukuu na wahakikishe chakula watakachonunua kiwe kilichohifadhiwa vizuri na kipo katika hali ya moto.

Amesema wamekuwa wakitoa elimu kupitia vyombo vya habari na mikutano ya hadhara juu ya kuchemsha maji na kujiepusha kununua chakula kilichowazi lakini bado baadhi ya wananchi wamekuwa hawatilii maanani suala hilo.

Katika kukabiliana na maradhi ya kuharisha na kutapika, Dkt. Dahoma amesema wanaendelea kutoa taaluma kwa kamati za Afya za shehia na kutoa vifaa vya kutunzia usafi  kwa kamati hizo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.