Afisa wa kituo cha kupigia akibandika bango linaloonesha kuwa ni kituo cha kuhesabia kura baada ya kukamilika kwa zoezi la upigaji kura tarehe 25/10/2015.
Afisa wa kituo cha kuhesabia kura akikata vifungio vya sanduku la kura huku akishuhudiwa na mawakala wa vyama vya siasa kwa ajili ya kuanza zoezi la kuhesabu kura.
Mawakala wa vyama vya siasa vilivyoshiriki Uchaguzi Mkuu wakishuhudia kwa makini zoezi la kuhesabu kura baada ya kukamilika kwa upigaji wa kura shehia ya Malind Mjini Zanzibar tarehe 25/10/2015.
Afisa wa kituo cha kuhesabia kura Malindi akizimwaga chini Karatasi za kura kwa ajili ya kuanza zoezi la kuhesabu kura.
Maafisa wa kituo cha kuhesabia kura wakihesabu kura za raisi Kwa jumla kabla ya kuzigawanya kwa mujibu wa vyama.
Maafisa wa kituo cha kuhesabia kura shehia ya Saateni wakihesabu kura kwa kuzigawa kwa kila mgombea kwa mujibu wa alivyopata.
No comments:
Post a Comment