Habari za Punde

ZEC/UNDP yaendesha Semina kwa asasi za kiraia kuhusu uchaguzi

Asasi za kiraia nchini zimeshauriwa kuchukua jitihada binafsi kutoa elimu ya uraia na elimu ya wapiga kura kwa jamii ili kila mwananchi aweze kutumia haki yake ya kidemokrasia ya kupiga kura kwa hali ya amani na utulivu.
Ushauri huo ulitolewa na kamishina wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Mh. Haji Ramadhani Haji huko Hoteli ya Bwawani Salama Hall wakati alipokuwa akifungua Semina ya Asasi za kiraia kuhusu masuala ya Uchaguzi,semina ambayo iliandaliwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar kwa kushirikiana na Shirika la umoja wa mataifa la mipango ya kimaendeleo (UNDP).
Mh. Haji aliendelea kwa kusema kwamba Tume ya uchaguzi Zanzibar itahakikisha kila mmoja anashiriki kupiga Kura kwa Kwani imeandaa njia madhubuti za kutoa elimu ya wapiga kura ikiwemo kufanya semina kwa wadau na kusambaza nyaraka za elimu hiyo kwa wananchi.
Nae mtaalamu wa Uchaguzi kutoka UNDP Bi Hamida Kibwana alizitaka asasi za kiraia kujaribu kuwahamasisha wanawake washiriki katika harakati za kiuchaguzi ikiwemo haki ya kupiga kura.
DSC03655
Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar akifunga semina ya asasi za kiraia tarehe 08.09.2015 Salama Hall hoteli ya Bwawani Zanzibar
Akifunga semina hiyo Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mh.Ayoub Bakar Hamadi alisema, Tume imeandaa mazingira mazuri  kuhakikisha watu wenye mahitaji maalum wanapatiwa msaada katika vituo vya kupigia kura na itatoa  vifaa maalum vya kupigia kura kwa watu wasiona ili nao waweze kupiga kura siku hiyo.
Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar inajukumu la kutoa elimu ya wapiga kura kwa mujibu wa sharia ya Uchaguzi No. 11 ya mwaka 1984.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.