Habari za Punde

Zoezi la Upigaji Kura likiendelea Zanzibar na Kujitokea Wananchi Wengi na Kuendelea kwa Amani na Utulivu katika Majimbo Yote ya Zanzibar.

 
Wananchi wa Jimbo la ShauriMoyo wakiangalia majina yao katika ubao wa matangozi katika Kituo cha Kupigia Kura cha Skuli ya Chekechea Saateni Zanzibar.
Mawakala wa Vyama vya Siasa katika Kituo cha Kupigia Kura cha Skuli ya Chekechea Saateni Zanzibar, wakifuatilia upigaji wa Kura katika kituo hicho.
Mwananchi wa Jimbo la Shaurimoyo akisubiri kuchukua kura yake kwa ajili ya kutumia nafasi yake ya msingi kumchagua Kiongozi wake katika Kituo cha kupigia Kura cha Skuli ya Maandalizi Saateni Zanzibar. 
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mhe Jecha Salim Jecha akiwa na wananchi wa Jimbo la Shaurimoyo wakiangalia majiya ya Wapiga Kura katika bango la picha za Wapiga kura Zanzibar.
Msimamizi wa Uchaguzi wa Kituo cha Skuli ya Saateni Jimbo la Shaurimoyo akiangalia jina na Mpiga Kura katika Daftari la Wapiga Kura wa Jimbo hilo.
Wananchi wa   Jimbo la Chumbuni Zanzibar wakiwa katika Kituo cha Kupigia Kura katika Skuli ya Muembemakumbi wakisubiri zamu zao kuweza kupiga kura kutumia haki zao za msingi kumchagua kiongozi wao.
Wananchi wa Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar wakiwa katika foleni wakisubiri kupiga Kura katika Kituo cha Skuli Kiembesamaki Zanzibar wakiwa katika hali ya Amani na Utulivu wakati wa zoezi hilo likiendelea katika vituo mbalimbali vya Zanzibar katika kupiga kura.
Mwananchi wa Jimbo la Kiembesamaki akisaidiwa na jamaa yake kwenda kupiga kura katika kituo cha Skuli ya Kiembesamaki Zanzibar.
Mwananchi wa Jimbo la Kiembesaki Zanzibar akipiga kura yake katika Kituo cha Kupigia Kura Kiembesamaki Zanzibar.
Mwananchi wa Jimbo la Kiembesamaki akiwekwa wino maalum baada ya kupiga kura yake katika kituo cha Skuli ya Kiembesamaki Zanzibar.
Mawakala wa Vyama vya Siasa Zanzibar wakiwa katika Kituo cha Kupigia Kura cha Kiembesamaki Zanzibar wakifuatilia zoezi hilo upigaji kura likiendelea katika vituo mbalimbali kwa Amani na Utulivu Zanzibar.
Mwananchi wa Jimbo la Kiembesamaki akipiga Kura yake katika Kituo cha Skuli ya Kiembesamaki Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Mohammed Gharib Bilal akiwasili katika viwanja vya Skuli ya Kiembesamaki kwa ajili ya kupiga kura yake, katika Kituo cha Kupigia Kura cha Skuli ya Kiembesamaki Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal akihakikiwa katika Daftari la Wapiga Kura katika Kituo cha Kiembesamaki Zanzibar. 
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Mohammed Gharib Bilal akipiga   kura yake katika Kituo cha Kupigia Kura cha Skuli ya Kiembesamaki Zanzibar. 
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Mohammed Gharib Bilal akitoka katika Kituo cha Kupigia Kura cha Skuli ya Kiembesamaki Zanzibar baada ya kupiga kura yake.
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Mohammed Gharib Bilal akizungumza na Waandishi wa habari Zanzibar baada ya kupiga kura yake. katika Kituo cha Kupigia Kura cha Skuli ya Kiembesamaki Zanzibar.
Waandishi wa habari wa Vyombo mbalimbali wakiwa katika kituo cha kupigia kura cha Skuli ya Kiembesamaki Zanzibar wakisubiri Viongozi wanaokuja kupiga kura katika kituo hicho.
 Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na msimamizi wa Kituo cha Kupigia kura cha Skuli ya Kiembesamaki Zanzibar akiwasili katika viwanja hivyo kwa ajili ya kupiga kura yake.  
 Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM Mhe Samia Suluhu Hassan, akipiga kura yake katika Kituo cha Kupigia Kura cha Skuli ya Kiembesamaki Zanzibar. 
Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM Mhe Samia Suluhu Hassan, akipiga kura yake katika Kituo cha Kupigia Kura cha Skuli ya Kiembesamaki Zanzibar. 
Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mgombea Uwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki kwa Tiketi ya CUF Mohammed Nassor.
Mgombea Mwenza wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akiwa na Mgombea Uwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar, Mhe Mahmoud Thabit Kombo wakitoka katika maeneo ya kituo cha kupigia Kura Skuli ya Kiembesamaki Zanzibar.
Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania CCM Mhe Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waandishi wa habari baada ya kupiga kura yake katika kituo cha Skuli ya Kiembesamaki Zanzibar. 
 Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ADA-TADEA Mhe Juma Ali Khatib, akitoka katika Kituo cha Kupigia Kura kilichoko Skuli ya Kiembesamaki Zanzibar. baada ya kupiga kura yake leo asubuhi. 
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ADA-TADEA Mhe. Juma Aki Khatib, akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali baada ya kupiga Kura yake katika Kituo cha Kupigia Kura cha Kiembesamaki Zanzibar na kueleza Uchaguzi unafanyika kwa Amani na Utulivu na Uko huru kwa wapiga kura hakuwa mtu aliyezuiliwa na kusukumwa katika kupiga kura yake. Na kusema atakubali matokea yakitangwaza kutoka na kuona hali nzuri ya upigaji Kura kwa mwaka huu. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.