Habari za Punde

Mratibu wa Mabadiliko Katika Sheria Msemo Mavare akizungumza wakati wa kuaza kwa ufunguzi wa Mafunzo hayo ya Siku Mbili ya Mabadiliko Katika Sekta ya Sheria Nchini yalioandaliwa na Wizara ya Katiba na Sheria Zanzibar.  
Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Sheria Zanzibar Mhe.Jaji Mshibe Bakari akifungua Mafunzo kwa Wakuu wa Idara za Sekretarieti ya Mabadiliko katika Sheria Juu ya Kusimamia Mabadiliko ya (Reforms) ya siku mbili yaliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar na kuwashirikisha Wadau wa Sheria na Wakuu wa Idara za Serikali Zanzibar kushoto ni Dr Natujwa Mvungi  kutoka Law School of Tanzania na Dr Julius Cosmas kutoka Kitivyo cha Sheria Mzumbe  waliotoka Mada kuhusu Mabadiliko Katika Sekta ya Sheria Nchini.

  
Mkurugenzi  Mipango, Sera na Utafiti wa Wizara ya Katiba na Sheria Zanzibar Daima Mohammed Mkalimoto, akitowa maelezo wakati wa mafunzo hayo  kwa washiriki kabla ya kuaza kwa mafunzo hao yaliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.


Mtoa Mada kutoka Chuo cha Mzumbe Kitivo cha Sheria Dr Julius Cosmas, akiwasilisha Mada inayozungumzia Mabadiliko Katika Sekta ya Sheria Ncnini wakatio wa mafunzo hayo ya Siku mbili yalioandaliwa na  Wizara ya Katiba na Sheria Zanzibar kwa Wadau wa Idara Serikali na Sheria Zanzibar, yaliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
Washiriki  wa Mafunzo ya Siku mbili Kwa Wakuu wa Idara na Sekretariet ya Mabadiliko  katika Sheria  wakifuatilia mafunzo hayo yaliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar
Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar Mhe Ibrahim Mzee akiwa na  Wakuu mbalimbali kutoka katika Idara na Taasisi za Sheria Zanzibar wakifuatilia Mada hiyo wakati ikiwakilishwa katika Mafunzo hayo ya Mabadiliko ya Sheria yalioandaliwa na Wizara ya Sheria na Katiba Zanzibar kwa Wadau wa Sheria Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.