MSAIDIZI mkutubi wa
Maktaba kuu ya Chake Chake Pemba Mwache Mohamed Bakari, akiwagawia vitabu
wanafunzi wa skuli ya msingi Kiuyu kipangani shehia ya kifundi Jimbo la Konde
Wilaya ya Micheweni, ikiwa ni lengo la uhamasihaji wanafunzi wa skuli za msingi
kupenda kusoma vitabu, katika utekelezaji wa mradi wa Out Reach Program
unaofadhiliwa na SIDA.
MWANAFUNZI Fatma
Ahmed Omar anayesoma darasa la sita katika skuli ya msingi Kiuyu Kipangani
shehia ya Kifundi Jimbo la Konde Wilaya Micheweni, akisoma risala ya usomaji wa
vitabu katika utekelezaji wa mradi wa Out Reach Program unaofadhiliwa na SIDA
MSAIDIZI mkutubi wa
maktaba kuu ya Chake Chake Pemba, Mwache Mohamed Bakari akiwaimbisha nyimbo
wanafunzi wa skuli ya msingi Kiuyu Kipangini shehia ya Kifundi Jimbo la Konde
Wilaya ya Micheweni, wakati wa utekelezaji wa mradi wa Out Reach Program
unaofadhiliwa na SIDA.
MSAIDIZI mkutubi wa
maktaba kuu ya Chake Chake Pemba, Mwache Mohamed Bakari akiwaonesha wanafunzi
wa skuli ya Msingi Kiuyu Kipangani, jinsi gani ya usomaji wa kitabu wakati wa
utekelezaji wa mradi wa Out Reach Program Unaofadhiliwa na SIDA.
MWANAFUNZI Seif
Khatib Mtwana akisoma taarifa ya skuli yake ya Kiuyu Kipangani jinsi inayotoa
huduma za maktaba, wakati wa utekelezaji wa mradi wa Out Reach Program
unaofadhiliwa na SIDA.
MSAIDIZI mkutubi wa
maktaba Kuu Chake Chake Pemba, Mwache Mohamed Bakari akiwaonyesha wanafunzi wa
skuli ya msingi Kiuyu Kipangani picha mbali mbali zinazopatikana maktba za
Pemba, wakati wa utekelezaji wa mradi wa Out Reach Program unaofadhiliwa na
SIDA.
MWANAFUNZI Asha
Khamis akitoa kitandawili kwa wenzake wakati wa uhamasishaji wanafunzi kutumia
makataba katika utekelezaji wa mradi wa Out Reach Program Unaofadhiliwa na SIDA
MWANAFUNZI Saumu
Rashid Haji wa darasa la kwanza katika skuli ya Kiuyu Kipangani, akijibu
chemsha bongo wakati wa uhamasishaji wanafunzi kutumia maktaba katika
utekelezaji wa mradi wa Out Reach Programa unaofadhiliwa na SIDA.
MWANAFUNZI Subira
Khalid Omar akisoma hadithi katika kitabua wakati wa uhamasishaji wanafunzi
kutumia maktaba kwenda kujisomea, katika utekelezaji wa mradi wa Out Reach
Program unaofadhiliwa na SIDA
WANAFUNZI wa skuli ya msingi Kiuyu Kipangani shehia ya kifundi
jimbo la Konde, wakichora picha mbali mbali katika utekelezaji wa mradi wa Out
Reach Program unofadhiliwa na SIDA.(Picha
na Abdi Suleiman, PEMBA.)
No comments:
Post a Comment