Habari za Punde

Usafi wa Mazingira Soko la Mwanakwerekwe Zenj.

Mfanyakazi wa Soko la Mwanakwerekwe Zanzibar akifanya usafi katika eneo hilo la soko ili kuliweka katika mazingira bora ya usafi.
Eneo la Mama Lishe limezoeleka kuwa na harakati za mchana kujipatia chakula kwa wafanyabiashara katika Soko hilo wakati wa asubuhi na mchana kwa sasa likiwa limefungwa. kuepusha maradhi ya mripuko wa matumbo. 
Eneo la Mama lishe katika Soko la Mwanakwerekwe Zanzibar limefungwa na Halmashauri ya Wilaya ya Magharibi kutokana na mazingira yake hayaridhishi kwa biashara ya chakula ikizingatiwa wakati huu wa mvua za vuli. 
Mfanyabiashara za Mitumba katika Soko la Mwanakwerekwe akiweka mchanga katika sehemu yake ya biashara kutokana na kutowama kwa maji ya mvua katika eneo lake la biashara. kama alivyokutwa na mpiga picha akiwa katika matembezi yake mitaani.    

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.