Habari za Punde

TOC yatoa mafunzo ya uongozi kwa Walimu wa skuli za Wilaya za Unguja

Mgeni Rasmi Vuai Khamis Juma ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara Ya Elimu na Uwendeshaji Zanzibar akifungua rasmi mafunzo hayo.


  
Rais wa Kamati ya Olympiki Tanzania TOC Gulam Abdalla Rashid akizungumza na Walimu wa Skuli mbalimbali hawapo pichani waliohudhuria Mafunzo ya uongozi,kushoto yake ni Mgeni Rasmi Vuai Khamis Juma pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Elimu, Utumishi na Uendeshaji na Maalim Khamis Khairalla, kulia ni Mjumbe wa TOC Mussa Abdurab. Mafunzo hayo yanafanyika Ukumbi wa Elimu Mbadala Rahaleo Mjini Zanzibar.
.

Rais wa TOC Gulam Abdalla Rashid akizungumza na Wajumbe mbalimbali waliohudhuria Mafunzo ya uongozi katika Ukumbi wa Elimu Mbadala Rahaleo Mjini Zanziba



Washiriki wa mafunzo ya uongozi yanayotolewa na Kamati ya Olympiki Tanzania TOC wakiwa katika Picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa mafunzo hayo huko katika Ukumbi wa Elimu Mbadala Rahaleo.
Picha na Abdallah Omar- Maelezo Zanzibar

Na Miza Othman / Rahma khamis -Maelezo    

Walimu wa Michezo katika Skuli mbalimbali wametakiwa kuirejesha Michezo kwa lengo la kukuza vipaji vya wanafunzi katika Skuli zao.

Kwa kufanya hivyo wataweza kurudisha ari na Vipaji mbalimbali vya wanafunzi ambao wanauwezo wa kuijengea heshima Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Idra ya Elimu Utumishi na Uendeshaji Vuai Khamis Juma alipokuwa akifungua mafunzo ya siku tano ya kamati ya wanamichezo Tanzania (TOC) katika Ukumbi wa Elimu mbadala Rahaleo mjini Zanzibar.

Amesema lengo la mafunzo hayo ni kurejesha haiba ya Michezo katika Skuli ili kuwawezesha wanafunzi kushiriki Michezo mbalimbali na kuendeleza vipaji.

Ameongeza kuwa kuwepo kwa Michezo hiyo pia kutasaidia kuwahamasisha Wanafunzi kupenda kubaki Skuli badala ya kutoroka kama wanavyofanya baadhi yao.

Mkurugunzi Vuai amefahamisha kuwa Michezo yote ni ajira nakwamba kama Wanafunzi watatumia vyema Vipaji vyao kutawapelekea kupata ajira na kupunguza tatizo la umasikini.

Aidha amefahamisha kuwa mafunzo hayo yamekuja muda muwafaka hasa ikizingatiwa kwamba Serikali imo katika mipango ya kuibua vipaji hivyo kwa lengo la kurejesha haiba ya michezo nchini.

Naye Rais wa kamati ya wanamichezo Tanzania Gulam Abdallah Rashid amesema Katamati itatumia busara kuhakikisha vijana wanashiriki katika michezo hiyo ikiwemo mashindano ya kitaifa na kimataifa.

Hata hivyo amesema watatafuta Waalimu wenye ujunzi wa kufundisha michezo hiyo ili kuhakikisha wanaibua wanamichezo waliobora na wenyevipaji katika skuli zao.

Vilevile amewaomba walimu waliopatiwa mafunzo hayo kushauriana na mamlaka husika ili kupatikana Viwanja vya Michezo katika kila Skuli za Zanzibar.
Aidha amewaomba Walimu hao kuhakikisha kuwa Viwanja hivyo vinalindwa na kutunzwa vyema ili visimilikiwe na baadhi ya watu wasiopenda maendeleo ya wanafunzi hao.

Sambamba na hayo Rais huyo amewataka washiriki wa mafunzo hayo kuto yakalia na badala yake kuyafanyia kazi ili kufikia malengo waliokusudia.

Mafunzo hayo ya siku tano yameshirikisha Walimu wa Skuli,Waratibu pamoja na Wakufuzi wa Michezo hiyo ambapo  Wilaya saba zimeshiriki katika Mkoa wa Mjini.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.