Mchapalo wa Maadhimisho ya Miaka 70 ya mkutano wa Kwanza wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Mkutano huo ulifanyika Januari 10,1946 katika Ukumbi wa Westminster, London Uingereza . Pichani anaonekana Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, akimpatia kipande cha keki, Sir Brian Urquhart aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Msaidizi Mwandamizi akishughulikia masuala ya Siasa na mmoja wa watumishi wa kwanza wa Sekretarieti ya Umoja wa Mataifa. Maadhimisho hayo yamefanyika siku ya jumatatu hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
Na
MwandishiMaalum, New York
Baraza
Kuu la Umoja wa Mataifa, jana jumatatu limeadhimisha
miaka 70 tangu mkutano wa kwanza wa Baraza hilo ulipofanyika January 10, 1946
hukoWestminister, London, Uingereza.
Pamoja
na kuzungumzia mafanikio na changamoto mbalimbali ambazo Baraza Kuu la Umoja wa
Mataifa limepita, moja ya jambo ambalo limebainika wazi ni uwiano mdogo wa idadi
ya mabalozi wanawake na wanaume wanao ziwakilisha nchi zao katika ngazi ya Wawakilishi
wa Kudumu.
Akizungumzia
tofauti hiyo, Rais wa Baraza Kuu la 70, Bw. Mogens Lykketoft, ambaye naye ametimiza
miaka70 ya kuzaliwa kwake Januari 10,
amesema“ Cha kuvutia, lakini na ambacho si cha kushangaza, sikuulipofanyikamkutanowa
kwanza wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa,hapakuwa na Mwakilishi wa Kudumu mwanamke.
Hali
hii inaendelea hadi sasa ambapo idadi ya wawakilishi wa wanawake haizidi asilimia
18”.
Wakati
huo mwaka 1946 nchi wanachama walioshiriki mkutano huo wa kwanza wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa zilikuwa 51. Miaka70 baadaye
Umoja wa Mataifa una nchi wanachama 193.
“Mkutano
ule wa kwanza ulikuwa na mambo mengi ya kuvutia,
kwanza ulidumu kwa saa moja, na ndani ya
muda huo, palipitishwa uamuzi mmoja tu nao ulikuwa ni wakumchagua Rais wa Baraza
hilo” amesimulia Bw. Lykketoft
Na
kuongeza“ Hata hivyo uamuzi huo ilibidi upigiwe kura. Bw. Tyrgve Halvdan Lie wa
Norway, alipoteza kura kwa Bw. Paul
Henri Spaak wa Ubeligiji. Hata hivyo Bw. Lie hakuhitaji kuwa na hofu sana kwani wiki tatu baadaye alikuja kuwa Katibu Mkuu wa
Umoja wa Mataifa.
Rais
wa Baraza Kuu la 70 ameeleza kwamba hapana shaka mkutano ule wa kwanza uliofanyika
mwaka 1946 uliweka msingi wa mambo mengi na ulikuwa mwanzo wa hatua muhimu wakile
kinachojulikana hivi sasa kama Jumuiya ya Kimataifa.
Akabainisha
pia kuwa,baada ya dunia kupitia misukosuko na matukio ya kutisha kama vile vita
kuuza dunia, uharibifu mkubwa, mauaji ya kimbali, ulipuaji wa mabomu ya nyukilia,
mataifa ya dunia yaliamua kwa makusudi kuwa kitu kimoja na kuchagua njia sahihi
ya kuifanya dunia iwe ya amani,usalama, haki, haki za binadamu na maendeleo ya kijamii.
“
Na katika Baraza Kuu, waliunda chombo cha kweli, chombo ambacho kila taifa liwe
dogo ama kubwa limeweza kuwa na sauti na sauti yake inasikilizwa” akasema Rais wa
Baraza Kuu. Huku akifafanua kwamba wakati huo wa mkutano wa kwanza,sehemu kubwa
ya dunia na hususani Afrika ili kuwa bado katika utawala wa kikoloni
“ Leo hii nchi wanachama ni 193 zikiwakilisha asilimia
99.5 ya idadi ya watu wote duniani, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa,limekuwa chombo chenye uwakilishi
jumuishi na chenye kutoa maamuzi kuhusu mambo mengi muhimu.
No comments:
Post a Comment