Habari za Punde

Naibu Katibu Mkuu Mambo ya Ndani ya Nchi Afanya Ziara Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)

Naibu Katibu Mkuu wa Wizaraya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (katikati), akiongozana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dickson Mwaimu (kulia), wakati alipotembelea kituo cha kumbukumbu cha Mamlaka hiyo, mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam. Kushotoni Mkurugenzi wa Uzalishaji Vitambulisho (NIDA), Paul Bwathondi.
Msimamizi wa Mifumo wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Ami Mohamed (kulia), akimuonyesha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kushoto), jinsi taswira ya muombaji kitambulisho inavyohifadhiwa kwenye mfumo ili kuwezesha kuiweka kwenye kitambulisho. Naibu Katibu Mkuu  alikuwa kwenye ziara ya kutembelea Mamlaka hiyo mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kulia),akiuliza swali baada ya kupata maelezo kutoka kwa Afisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Noel Chikwindo (kushoto), Naibu Katibu Mkuu alikuwa kwenye ziara ya kutembelea Mamlaka hiyo mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (aliyenyooshamkono), akifuatilia kwaumakini uhakiki wa taarifa za muombaji wa Kitambulisho cha Utaifa, wakati alipotembelea kitengo cha Uhakiki waTaarifa cha Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Kulia ni Mkurugenzi wa Uzalishaji Vitambulisho, Paul Bwathondi .Naibu Katibu Mkuu alikuwa kwenye ziara ya kutembelea Mamlaka hiyo mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Uzalishaji Vitambulisho wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Paul Bwathondi (kulia), akitoa ufafanuzi kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya  Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (watatu kutoka kulia waliosimama), Naibu Katibu Mkuu alikuwa kwenye ziara ya kutembelea Mamlaka hiyo mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kulia), akielezea jambo wakati alipotembelea Kitengo cha kudhibiti ubora wa Vitambulisho vya Taifa, kilichopo kwenye Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA),Katikati ni Mkurugenzi wa Uzalishaji Vitambulisho, Paul Bwathondi na kushoto ni Afisa Usajili anayeshughulikia ubora, Jemima Mulokozi. Naibu Katibu Mkuu alikuwa kwenye ziara ya kutembelea Mamlaka hiyo mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam.
Afisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), anayeshughulikia ubora, Jemima Mulokozi (kushoto), akimuelezea Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kushoto), jinsi wanavyothibiti ubora wa Kitambulisho cha Utaifa kabla akijachapishwa.Naibu Katibu Mkuu alikuwa kwenye ziara ya kutembelea Mamlaka hiyo mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam.
( (Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikalini-Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.