Habari za Punde

Shamrashamra Maadhimisho ya Sherehe za M,apinduzi Zanzibar Kutimia Miaka 52 kwa Uzinduzi Miradi Mbalimbali Zanzibar

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akiwasili katika bandari ya Mkokotoni Unguja kwa ajili ya kwenda kisiwa cha Tumbatu kuzindua Mradi wa Maji kwa Wananchi wa Kisiwa hicho.
 Makamu wa Pili wa Rais  wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwasili katika bandari ya Tumbatu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Wananchi wa Kisiwa cha Tumbatu alipowasili katika Kisiwa hicho.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Wazee wa Kisiwa cha Tumbatu.
 Wananchi wa Kisiwa cha Tumbatu wakiwa katika bandari hiyo wakimpokea Makamu wa Pili wa Rais alipowasili katika bandari hiyo kwa ajili ya Uzinduzi wac Mradi wa Maji Kisiwani humo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) Dk Mustafa Ali Garu akitowa maelezio ya ukamilikaji wa mradi huo wa usambazaji wa maji katika kisiwa cha Tumbatu kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati wa shamrashamra za sherehe za Mapinduzi kutimia miaka 52, uzinduzi huo umefanyika kisiwa cha Tumbatu Unguja. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali  Iddi akizungua Mradi Mkubwa wa Maji Safi na Salama kwa Wananchi wa Kisiwa cha Tumbatu Unguja akifungua kipazia kuashiria uzinduzi wa Mradi huo katika Kisiwa hicho, ikiwa ni shamrashamra za sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali  Iddi akizungua Mradi Mkubwa wa Maji Safi na Salama kwa Wananchi wa Kisiwa cha Tumbatu Unguja akifungua mfereji kuashiria uzinduzi wa Mradi huo katika Kisiwa hicho, ikiwa ni shamrashamra za sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.