Habari za Punde

Wakaazi wa Kata ya Namayuni Waipongeza Mtandao wa Simu za Mkononi wa HALOTEL

Afisa habari wa kampuni ya mtandao wa simu za mkononi ya Halotel, Frank Mwakyoma akizungumza na wananchi wa kijiji cha Namayuni kilichopo kata ya Namayuni Kilwa Masoko Mkoani lindi mara baada ya wafanyakazi wa kampuni hiyo kuwatembelea katika kijijini hapo.
Afisa habari wa kampuni ya mtandao wa simu za mkononi ya Halotel, Frank Mwakyoma akizungumza na wananchi wa kijiji cha Namayuni kilichopo kata ya Namayuni Kilwa Masoko Mkoani lindi mara baada ya wafanyakazi wa kampuni hiyo kuwatembelea katika kijijini hapo.

Diwani wa Kata ya Namayuni iliyopo Kilwa Masoko Mkoani Lindi, Hussein Sungura akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wakazi wa kijiji cha Namayuni mkoani humo walipotembelewa na Kampuni ya Simu za Mkononi ya Halotel ambayo ndio mtandao pekee uliowafikia wananchi na wakazi wa kata hiyo. 
Wakazi wa Kijiji cha Namayuni wakipata maelekezo walipo tembelea kibanda cha kusajili laini jijini  hapo.
Mtaalamu wa masuala ya mtandao  wa kampuni ya Halotel, Kilwa Masoko Mkoani Lindi, Sebastian Inocent akifafanua changamoto mbalimbali zinazo wapata wakazi wa kijiji cha Namayuni.

Na Mwandishi Wetu Lindi.
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Halotel ndio mtandao pekee unaotoa huduma za mawasiliano kwa njia ya Simu za mkononi katika kata ya Namayuni iliyopo Kilwa Masoko Mkoani Lindi.


Mtandao huu ndio unawasaidia wakazi wa kata ya Namayuni kuweza kuwasiliana na ndugu na jamaa  wa maeneo hayo na sehemu nyingine kwa njia ya simu ya mkononi kwa kuwa wamejengewa mnara unao wawezesha kuwasiliana kwa njia simu za mkononi.

 Diwani wa Kata ya Namayuni iliyopo Kilwa Masoko Mkoani Lindi, Hussein Sungura amepongeza mtandao wa simu za mkononi wa Halotel na kusema kuwa umeisaidia sana jamii ya wakazi wa kata ya Namayuni mkoani humo kutokana na hapo awali kutokuwepo na mtandao wowote wa simu.

"Tunawashukuru sana Kampuni ya simu za mkononi ya Halotel kukumbuka kama kunaviumbe huku na kutuwekea mnara katika kata yetu kwakua kabla ya mtandao huu tulisafiri na kupanda juu ya vilima ili kutafuta mtandao(network) ili tuweze kuwasiliana na watu wengine kwa njia ya simu"


Nao wakazi wa Kijiji cha Namayuni wamesema kuwa Mtandao huu wa Halotel "umetusaidi sana katika huduma mbalimbali hasa kutufichia siri katika mawasiliano kwani tulikuwa tunaenda umbali mrefu kwenda kutafuta mtandao, kwa sasa tunakaa ndani tuu na tunawasiliana na ndugu na jamaa  bila mtu yoyote kujua kama tumewasilana na nani"


 Wafanyakazi wa mtandao wa Halotel wametembelea kata  ya Namayuni kwaajili ya Kampeni ya HALO MAISHA inayoendelea katika maeneo mbalimbali  yaliyofikiwa na mtandao huo nchi zima ili kila jamii ifaidike na spidi kubwa ya intaneti na upatikanaji wa huduma nzuri za mtandao huo.


Kampuni ya Halotel  ambayo ina mpango wa kuwafikia asilimia 95 ya watanzania hadi ifikapo mwishoni mwa mwaka huu na kauli mbiu yao ya Pamoja katika Ubora, inalenga kuhakikisha kila mtanzania anakuwa na simu ya mkononi pamoja na kupata huduma ya mtandao kwa kila sehemu ya Tanzania, ambapo mpaka sasa imeshaunganisha mtandao wa simu kwa zaidi ya vijiji 1500 ambavyo vilikuwa havijaunganishwa na huduma ya mtandao wowote wa simu kutoka mwanzo.
Katika hatua nyingine, kampuni ya Halotel itaweka mkazo wa hali ya juu katika kuboresha mtandao, huduma kwa wateja, huduma kwa jamii hali itakayopelekea mapinduzi katika sekta ya mawasiliano nchini.
Ikiwa na kilomita 18,000 za fibre optic, pamoja na zaidi ya minara 2500, Halotel ndiyo kampuni yenye mtandao mkubwa zaidi nchini, ambayo pia itatumika kuunganisha serikali za mitaa 150, hospitali 150, vituo vya polisi 150, ofisi za posta 65 na intaneti ya bure kwa shule zaidi ya 450.
Hadi sasa Halotel imeshawekeza zaidi ya dola bilioni 1 za kimarekani mpaka sasa kwa kutengeneza miundombinu na kuboresha mtandao wa mawasiliano, kampuni ya Halotel imefanikiwa kufikisha huduma za mtandao katika mikoa yote 26 nchini, pamoja na miji na vijiji, ikiwa ni zaidi ya asilimia 95% ya watanzania wote hivyo kuifanya kuwa kampuni yenye mtandao mkubwa zaidi nchini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.