Habari za Punde

Kituo cha Huduma za Sheria Pemba Chatoa Elimu ya Sheria kwa Vikundi vya Ushirika Pemba.

Afisa Mdhamini Wizara ya Katiba na Sheria Pemba, Omar Khamis Juma akifungua mafunzo ya elimu ya uraia, kwa viongozi wa asasi za kirai za Mkoa wa kusini Pemba, kulia ni Mratib wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC, tawi la Pemba Fatma Khamis Hemed, ambao ndio waandaji wa mafunzo hayo, na kushoto ni mratibu wa mafunzo hayo Mohamed Hassan Ali
Baadhi ya Viongozi wa Asasi za Kiraia Mkoa wa Kusini Pemba, wakifuatilia mafunzo ya elimu ya uraia, yaliofanyika na kuandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC Tawi la Pemba
 Mtoa Mada ya Ufafanuzi wa Katiba,Bi.Fatma Khamis Hemed kutoka Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC Tawi la Pemba, akimuuliza suali la ‘nini maana ya katiba’ mmoja kati ya viongozi wa NGOs mkoa wa kusini Pemba, kwenye mafunzo ya elimu ya uraia yalioandaliwa na ZLSC
 Mtoa Mada ya Mgawanyo wa Madaraka Ndg.Mohamed Hassan Ali, kutoka Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, akiwasilisha mada hiyo, kwenye mafunzo ya elimu ya uraia kwa viongozi wa NGOs mkoa wa kusini Pemba, kwenye mafunzo ya elimu ya uraia yalioandaliwa na ZLSC.
Afisa Uhamiaji wa mkoa wa kaskazini PembaNdg. Omar Said Mohamed, akiwasilisha mada ya ‘nani raia’ kwenye mafunzo ya elimu ya uraia yalioandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, kulia ni mratib wa mafunzo hayo Mohamed Hassan Ali, mafunzo hayo yalifanyika mjini Chakechake.
Mtoa Mada ya utawala bora, utawala wa sheria na Demokrasia,Ndg.Khalfan Amour Mohamed, kutoka Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, akiwasilisha mada hiyo, kwenye mafunzo ya elimu ya uraia kwa viongozi wa NGOs mkoa wa kusini Pemba, mafunzo yalioandaliwa na ZLSC, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.