Habari za Punde

Historia Yajiridua Kisiwani Pemba Katika Mchezo wa Jamhuri na Chipukizi Kukutana Katika Uwanja wa Gombani Kesho.

Mchezo wa Timu hizo uliofanyika wakati wa Enzi zao walipokutana katika Mchezo wa Ligi Kuu ya Zanzibar Grand Malt Katika Mchezo huo Timu ya Chipukizi imeibuka na Ushindi wa Mabao 3--0. Nani katika mchezo huo wa kesho ataibuka kudedea?
Nahodha wa timu ya Jamhuri Mfaume Shaaban (29) akijaribu kumzuia mshambuliaji wa timu ya Chipukizi Faki Mwalimu. Wakati wa mcezo wao wa ligi Kuu ya Zanzibar ‘Grand Malt’ uliochezwa uwanja wa Gombani. Chipukizi iliibuka na ushindi wa magoli 3-0 mawili yakifungwa na mshambuliaji huyo.

Jumanne ya Machi 15, mwaka huu wa 2016 itaingia kwenye historia ya wapenda soka na hasa kule kisiwani Pemba wakati vilabu vya ligi vitakapoanza kushuka viwanjani.

Licha ya mvutano uliokuwepo kwa vilabu hivyo kuweka mgomo wa kutoingia viwanjani kwa madai ya kutoitambua kamati ya mpito iliyoundwa mafichoni lakini Mungu ameleta kudra na kuwapa moyo viongozi wa vilabu hivyo kupunguza munkar baada ya kuona mambo yameanza kukaa sawa.

Unapoiyangalia ratiba ya ligi hiyo utagundua kuwa siku hiyo kutakua na michezo miwili ambapo Al-Jazira iliyopanda daraja itacheza na timu kongwe ya Kizimbani kwenye dimba la FFu Finya.

Kiukweli pambano hili linatarajiwa kuwa na upinzani kiasi kutokana na timu zote mbili kutokea mji wa Wete.

Ratiba hiyo pia inaonyesha kuwa kwenye dimba la Gombani timu konge ya Jamhuri iliyoanzishwa mwaka 1953 itachuana na Chipukizi.

Mchezo huu bila shaka yoyote ndiyo utakaobeba mashabiki wengi mbali ya kuwa ni timu za miji tofauti ya Wete na Chake Chake lakini pia kutokana na kuwa timu zilizowahi kucheza ligi kuu ya soka Zanzibar msimu wa 2012-2013 na kuteremka daraja.

Jamhuri na Chipukizi zilikutana September 17, 2012 kwenye ligi kuu ya soka ya Grand Malt Zanzibar na majogoo ya Wete walikubali kichapo cha bao tatu kwa bila huku mabao mawili ya Chipukizi yakifungwa na mpachika mabao Faki Mwalim ambaye kwa sasa ametua ndani ya klabu ya KMKM.
.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.