HOTUBA
YA MHESHIMIWA OMARI YUSUF MZEE, WAZIRI WA FEDHA WA SERIKALI YA MAPINDUZI
ZANZIBAR, KATIKA SHEREHE ZA UFUNGUZI WA TAWI JIPYA LA BANK OF AFRICA TANZANIA-
ZANZIBAR TAREHE 3 MACHI 2016
Balozi Mwanaidi
Sinare Maajar, Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi wa BANK OF AFRICA - TANZANIA
Ndugu Ammish Owusu-Amoah,
Mkurugenzi mtendaji wa
BANK
OF AFRICA - TANZANIA;
Wakurugenzi wa Bodi;
Wafanyakazi wa BANK
OF AFRICA - TANZANIA;
Wageni waalikwa;
Ninayo furaha kubwa
kuwa nanyi leo wote mliojumuhika
hapa kushiriki katika sherehe hii ya uzinduzi
wa Tawi jipya la
BANK OF AFRICA ZANZIBAR. Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu
kwa siku hii njema na kwa kutupa uwezo wa kuwa hapa leo. Napenda kuwashukuru
pia viongozi wote wa BANK OF AFRICA kwa kunipa heshima hii kubwa ya kuzindua
Tawi hili siku hii ya leo. Kwa dhati kabisa nawapongeza wote walioshiriki katika mchakato mzima wa kufanya tathmini na hatimaye kuamua kufungua Tawi la
BANK OF AFRICA hapa Zanzibar.
Kipekee nawashukuru Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi, Balozi Mwanaidi Sinare Majaar na
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki, Bwana Ammish Owusu- Amoah kwa jitihada zao kubwa za kutoa msukumo wa kuanzishwa
kwa Tawi hili. Nawashukuru na kuwapongeza wote. Nitumie nafasi hii pia kuwapa
hongera wananchi wa Zanzibar kwa kupata tawi la BANK OF AFRICA. Hongereni sana!
Leo ni siku adhimu na
ya kipekee ambapo tunashuhudia ufunguzi wa Tawi hili jipya la BANK OF AFRICA
ambalo litakuwa Tawi la kwanza hapa Zanzibar. Ni dhahiri kwamba ufunguzi wa Tawi hili ni ishara kwamba BANK OF AFRICA - TANZANIA imedhamiria kupanua
shughuli za kibenki nchini hasa katika kukuza uchumi wa Zanzibar.
BANK OF
AFRICA inakuja na mengi mpya katika Sekta ya Benki na kuleta huduma za kibenki
karibu na wananchi wa Zanzibar ikiungana na Benki zingine pamoja na
kushirikiana na BENKI KUU YA TANZANIA.
Wageni waalikwa,
Serikali inatambua kwamba
maendeleo yetu hususan ya kukuza uchumi na kuondoa umaskini hayawezi kuwa na
mafanikio bila ya kuhusisha Sekta binafsi. Hii ndiyo sababu katika miaka ya
1980 Serikali ilifanya juhudi kubwa katika kubadili Mfumo wa Uchumi kutoka
Mfumo Hodhi wa Dola kwenda Mfumo wa Soko Huria.
Katika mabadiliko hayo pia
kulifanyika mageuzi katika Sekta
mbalimbali ikiwemo Sekta ya Fedha. Uamuzi wa
BANK OF
AFRICA - TANZANIA kuwekeza kwenye upanuzi wa huduma
zake hapa Zanzibar,
ni utekelezaji thabiti wa dhamira ya Serikali ya kuvutia uwekezaji wa ndani na
nje ili kukuza Uchumi kwa kasi zaidi.
Vilevile, tumekuwa
tukifanya mageuzi mbalimbali tangu miaka ya1990 kwa mtazamo wa kuiwezesha
Sekta Binafsi kuwa ya muhimu sana katika Ukuaji wa Uchumi wetu. Katika miaka ya
hivi karibuni Serikali inajivunia kwamba tangu kuingia kwa Mfumo wa Soko Huria
hapa Nchini, Sekta Binafsi imeweza kuchukua nafasi yake na kuwekeza katika
huduma mbalimbali zikiwemo huduma za Sekta ya Fedha.
Serikali itaendelea
kuhakikisha uhusiano wa karibu uliopo kati ya Serikali na Sekta Binafsi
zikiwemo Taasisi za Fedha unakuwa uhusiano wa kudumu. Tutaendelea kuheshimu
mchango wa Sekta Binafsi ambao ni kichocheo kikubwa kwa Uchumi na maendeleo ya
Taifa letu. Serikali itaendelea na jukumu lake la kuboresha mazingira ya
uwekezaji ili kuhamasisha wawekezaji zaidi Nchini.
Pamoja na jitihada hizo bado
kuna maeneo yanayohitaji kuboreshwa ili kujenga mazingira bora ya Sekta Binafsi
kukua hasa suala la upatikanaji wa huduma za Kibenki Vijijini na katika Sekta
ya Kilimo. Nafurahi BANK OF AFRICA mmeanza vizuri kuisaidia Serikali kuleta
maendeleo katika huduma za Benki hapa Zanzibar.
Wageni waalikwa,
Napenda
kuwahakikishia kwamba serikali inafanya kila iwezalo katika kuhakikisha huduma
za kifedha zinamfikia kila Mzanzibari kwa urahisi kabisa. Katika kuhakikisha
hili linafanyika serikali ya Zanzibar inafanya ujenzi na uboreshaji wa miundombinu
hasa barabara, njia za mawasiliano na utengenezaji wa Sera zilizo stahiki.
Hii ni pamoja pia na kupigana na umasikini na
ukosefu wa
elimu kwa wananchi wa Zanzibar.
Nimekuwa nikiangalia
na pia kutokana na maelezo niliyopewa na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugeni, ni
kwamba katika miaka hii tisa BANK OF AFRCA imekuwa na uwezo wa kufungua matawi 22 sasa pamoja na Tawi maalum kwa ajili ya wateja wakubwa pale Dar es Salaam.
Pamoja na hili utaona kwamba matawi mengine yameenda ndani zaidi katika maeneo
ambayo upatikanaji wa huduma za kibenki ni adimu. Benki imetengeneza huduma za kipekee zakumfaa kila mmoja wetu ambazo pia zinapunguza ugumu wa utumiaji wa
huduma za kibenki kwa watu binafsi,wenye biashara ndogondogo, wenye vikundi,
wafanyabiashara za
kati na hata wafaya biashara wakubwa.
Wageni waalikwa,
Sasa ni wakati wa
Zanzibar kutumia huduma hizi zinazotolewa na BANK OF AFRICA, ili kupata
maendeleo yale tunayoyahitaji.
Wazanzibari hizi ndizo fursa, tusizifumbie
macho. Wale
wakulima,wavuvi, wenye mahoteli, wafanya biashara na vijana, sasa
ni wakati wa kutumia fursa hizi.
Nimeambiwa kwamba Tawi
limepata mapokezi ya kipekee kutoka kwa watu wa Mlandege na natumaini kwamba
heshima ambayo benki imejijengea katika miaka yake tisa ndani ya Tanzania bara itaenea pia Zanzibar. Na pia natumaini Zanzibar hatutobaki na tawi hili moja la
BANK OF AFRICA bali yataongezeka matawi mengi zaidi.
Wageni waalikwa,
Niombe uongozi pamoja
na wafanyakazi wote wa BANK OF
AFRICA kuhakikisha kwamba wateja wa Tawi hili la
Zanzibar
wanapata huduma za kipekee katika viwango vya kimataifa
tukiweka
pamoja na mahitaji ya Wazanzibari katika benki yenu.
Natumaini kuwa una
wafanyakazi wenye sifa, uwezo na weledi wa kufanya kazi na hivyo unachohitaji
sasa ni wateja.
Kwa haya machache,
kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar, naomba nichukuwe nafasi hii
kufungua rasmi na
kutambua Tawi jipa la BANK OF AFRICA ZANZIBAR.
Niwashukuru tena wote
kwa kuhudhuria tukio hili la kihistoria
kwa Zanzibar na nawakaribisha wote kuwa
wateja wa BANK
OF AFRICA.
Asante.
No comments:
Post a Comment