Habari za Punde

Kuapishwa kwa Spika wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zubeir Ali Maulid.


Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Dk Yahya Khamis Hamad akiingia katika Ukumbi wa Mkutano kutangaza Matokeo ya Kura ya Spika wa Baraza baada ya kumalizika kwa Uchaguzi na kuhesabiwa kura. zilizopigwa na Wajumbe Wateule wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar. 
Wajumbe Wateule wakiwa wamesimama wakati wa Kuingia kwa Katibu wa Baraza kuendelea na Kikao hicho kutowa matokeo ya Uchaguzi wa Spika. 
Mgombeav Uspika wa Baraza la Wawakilishi akiingia Ukumbini baada ya kutangaza mshindi wa nafasi hiyo ya Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe Zuberi Ali Maulid kwa ushindi wa kura 75 na kura moja imeharibika.
Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Dk Yahya Khamis Hamad akitowa maelezo kabla ya kumuapisha Spika mteule Mhe Zuberi Ali Maulid kwa kushinda katika uchaguzi huo kwa kura nyingi. zilizopigwa na Wajumbe Wateuli wa Baraza la Wawakilishi.
Katibu wa Baraza la Wawakilishi Dk Yahya Khamis Hamad akimuapisha Spika Mpya wa Baraza la Tisa Mhe Zuberi Ali Maulid baada ya kutangazwa mshindi wa nafasi hiyo ili kuliongoza Baraza la Wawakilishi kwa Kipindi cha Miaka Mitano.
Spika wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid akikata utepe Katiba ya Zanzinar na Tanzania na Kanuni ya Baraza la Wawakilishi baada ya kukabidhiwa na Katibu wa Baraza Dk Yahya Khamis Hamad baada ya kumalizika hafla ya kumuapisha. 
Spika wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Mhe Zuberi Ali Maulid akitowa shukrani kwa Wajumbe Wateuli wa Baraza la Wawakilishi kwa kumpigia Kura kuweza kuliongoza Baraza hilo kwa kipindi cha miaka mitano. 

Wajumbe Wateule wa Baraza la Wawakilishi wakiwa katika Ukumbi wa Mkutano. 
Makamu wa Pili wa Rais Mteule na Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Mhe Balozi Seif Ali Iddi na wajumbe wengine wakimsikiliza Mhe Spika Zuberi akitowa shukrani zake na kuahidi ushirikiano na Wajumbe wa Baraza katika Kazi zake za Vikao vya Baraza la Wawakilishi Zanzibar. 
Wajumbe Wateule wa Baraza la Wawakilishi wakimsikiliza Mhe Spika Zuberi Ali Maulid akitowa shukrani zake kwa Wajumbe hao baada ya kumpa ushindi wa kishindo.

Katibu wa Baraza Dk Yahya Khamis Hamad akiwa na wasaidizi wake katika ukumbi wa mkutano wakati Mhe Spika Zuberi akitowa shukrani kwa Wajumbe wa Baraza.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.