Mkurugenzi wa Idara ya Michezo na Utamaduni Zanzibar
Hassan Tawakal, akizungumza na walimu wa michezo Maskulini juu ya malengo na
mikakati ya Idara yake, katika kuhakikisha michezo maskuli inarudi tena huko
katika skuli ya madungu maandalizi Chake Chake Pemba.
AFISA Mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali
Pemba, Salum Kitwana Sururu akiwasisitiza walimu wa michezo maskuli,
kuhakikisha wanafuata kanuni na sheria za michezo, wakati wa mashindano ya
elimu bila ya malipo kikao hicho kimefanyika katika skuli ya Maandalizi Madungu
Chake Chake Pemba.
Mkurugenzi wa Elimu Mbadala na Mafunzo ya Watu wazima Zanzibar, Mashavu Ahmada Faki, akizungumza na walimu wa michezo Maskulini na Maafisa juu ya Maandalizi ya
Tamasha la Elimu Bila ya Malipo Zanzibar yanayotarajiwa kuadhimishwa mwezi wa Septemba kila mwaka, mkutano huko umefanyika katika
ukumbi wa skuli ya madungu maandalizi Chake Chake Pemba.
(Picha na Abdi Suleiman, Pemba.)
No comments:
Post a Comment