Habari za Punde

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe Charles Azungumza na Waandishi wa Habari Hali ya Amani na Utulivu Wakati wa Uchaguzi wa Marudui Zanzibar.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Tanzania Mhe. Charles Kitwanga akiwasili katika jengo la Afisi ya Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Zanzibar kwa ajili ya Mkutano wake na Waandishi wa Habari Zanzibar.
Waziri Kitwanga akizungumza na Waandishi wa habari ya ya Zanzibar wakati wa zoezi la Uchaguzi wa Marudio uliofanyika March 20, 2016 jumapili. Katika Uchaguzi huo hali ilikuwa ya utulivu na Amani kwa kipindi chote cha Uchaguzi na kusisitiza hali hiyo itaendelea kuwa ya Amani na Utulivu na Jeshi la Polisi litahakikisha hali hiyo itaendelea kwa siku zote kwa Wananchi wa Zanzibar kuwataka kudumisha amani.  

Waziri Kitwanga akizungumza wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Kilimani Zanzibar.

Waandishi wakifuatilia mkutano huo wa Waziri akitowa Taarifa kuhusiana na hali ya utulivu katika kipindo cha zoezi la Uchaguzi wa Marudio Zanzibar.




Mwandishi akimuuliza swali Mhe Waziri wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari katika Ofisi ya Makao Makuu ya Polisi Kilimani Zanzibar.
Waandishi wakiuliza maswali kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Tanzania, wakati wa mkutano huo.  
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe Charles Kitwanga akisisitiza jambo wakati akijibu maswali ya waandishi waliouliza wakati wa mkutano huo uliofanyika Makao Makuu ya Polisi Kilimani Zanzibar.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Tanzania Mhe Charles Kitwanga, akitoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Zanzibar baada ya kumaliza Mkutano wake na Waandishi wa Habari Zanzibar kuhusiana na hali ya Amani inavyoendelea Zanzibar wakati wa Uchaguzi wa Marudio uliofanyika march 20, 2016 na kusisitiza hali itaendelea Zanzibar kuwa Nchi ya Amani kwa Wananchi wake na ulinzi wa Jeshi la Polisi utaendelea hali hiyo inaendelea katika Visiwa vya Unguja na Pemba.   

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.