Habari za Punde

Barabara ya Mwanakwerekwe Imeshindwa Kupitika Kutokana na Mvua Barabara hiyo kufunikwa kwa Maji.

Barabara Kuu ya Mwanakewrekwe kuelekea Fuoni ikiwa imefunikwa na maji na kutanda gugu maji kutanda katika barabara hiyo baada ya kuzidiwa ziwa la Mwanakwerekwe kujaa maji hadi kufikia katika barabara hiyo na kukatisha gari za abiria ziendazo Fuoni kuishia Ng'ambu ya pili Makaburini na abiria wa eneo hilo kutembea kwa miguu. 
Wananchi wakiwa upande wa pili wa barabara hiyo eneo la kwerekwe Sokoni wakiangalia hali halisi ya kufurika kwa ziwa la mwanakwerekwe hadi kufunika barabara hiyo na kuleta madhara kwa wananchi na mali zao kuharibika kwa kujaa kwa maji hayo.

Baadhi ya bidhaa zikiwa zimeopolewa katika maji eneo hilo lilikuwa na wafanyabiashara wakifanya biashara zao kando ya barabara hiyo.
Moja ya gari iliokuwa emeegeshwa katika eneo la jirani ya barabara hiyo na kufunikwa na maji likifanyiwa matengenezo kutokana na kuingia maji katika mashine, gari nyigi zilikuwa zimeegeshwa katika moja ya sheli katika barabara hiyo zimeathirika na maji ya mvua na kuopolewa kwa kuvutwa hadi upande wa pili wa barabara na kufanyiwa mategenezo.ili kurudi hali yake.
Hili ndilo eneo lililopita barabara ya mwanakwerekwe kuelekea fuoni likiwa limefunikwa na maji na kutanga gugu maji likiwa limeota likitokea katika ziwa la mwanakwerekwe.
Mfanyabiashara akihamisha bidhaa zake kutoka dukani kutokana na kujaa kwa maji katika eneo la Mwanakwerekwe Unguja.
Baadhi ya bidhaa zikiwa zimeopolewa katika janga hilo la kujaa kwa maji eneo la maduka ya Mwanakwerekwe jirani na barabara hiyo.


Baadhi ya Wananchi wa maeneo ya fuoni wakipita njia ya nyumba mbili kuelekea fuoni ikiwa ni njia hiyo inayopitika baada ya kupungua kwa maji katika daraja hili wakati wa asubuhi likiwa limefunikwa na maji yanayopita eneo hilo kuelekea katika bwawa la Mwanakwerekwe.
Wananchi wakipita katika daraja la barabara ya nyumba mbili kuelekea mjini njia hiyo ikiwa na msongamano wa magari na watembea kwa miguu.Polisi wa Usalama Barabarani walifanya kazi ya ziada kuongoza magari katika eneo hilo.

2 comments:

  1. Ni muda wa kila MTU kujifanya engineer na kutoa matamko, mvua zikiptita hakuna liwalo.

    ReplyDelete
  2. Tatizo watu wamejenga ovyo eneo hilo. Zamani kulikuwa na mtaro, ambapo mvua ikinyesha maji yalikuwa yakienda moja kwa moja baharini.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.