Habari za Punde

Mkutano wa Kongano Bunifu la Wakulima wa Mwani Zanzibar Chini ya Ufadhili wa Milele Zanzibar.

Katibu wa Kongano la Mwani Zanzibar Ndg Rajab Ally (Lee)akitowa maelezo kabla ya kuanza kwa Mkutano huo wa Pili wa Kongano la Ubunifu wa Kilimo cha Mwani Zanzibar uliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Kilimo Maruhubi Zanzibar.
Mwanafunzi kutoka Chuo cha Royal Institute of Technoligy Sweden, Ida Stadenberg na Dan Neren kutoka Bilateral Assiciate Expert COSTECH Tanzania Commision for Scien Tech Dar es Salaam wakishiriki katika Kongano hilo la Mwani Zanzibar.

Naibu Katibu Mkuu iliyokuwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dk Omar Amir akifungua Kongano hilo la Bunifu la Mwani Zanzibar lililowashirikisha Wajasiriamali wa Kilimo cha Mwani Zanzibar, lililofadhiliwa na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Milele Zanzibar, lililofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Kilimo Maruhubi Zanzibar.kulia Mratibu Uchumi Jamii wa Milele Foundation Zanzibar Bi Alice Mushi na kushoto Dkt Flower Msuya Mtafiti wa Mwani Zanzibar. kutoka Taasisi ya Uchunguzi wa Baharini Zanzibar. 
Wakulima wa Mwani Zanzibare wakifuatilia ufunguzi wa Mkutano wao wa Kongano la Pili la Bunifu wa Mwani Zanzibar. wakiwa katika ukumbi wa mkutano.
Mratibu Uchumi Jamii wa Milele  Zanzibar Foundation, Bi Alice Mushi akitowa maelezo mafupi kutoka katika Shirika lake la Milele kuhusiana na kuwainua Wakulima wa zao la Mwani Zanzibar, wakati wa Kongano hilo la Wajasiriamali wa Kilimo cha Mwani Zanzibar.
Mratibu wa Mwani Zanzibar, Dkt Flower Msuya alitowa maelezo mafupi ya lengo la Mkutano huo kilichofanyika wakati wa mkutano wa kwanza uliopita na kutowa maelezo ya Mkutano wa Kimataifa wa Kisayansi wa Kilimu cha Mwani Duniani uliofanyika Nchi Marekani. 
Wakulima wa Kilimo cha Mwani na Maofisa wanunuzi wa Makampuni ya Mwani Zanzibar wakifuatilia Mkutano huo wa Kongamano Bunifu. 
Mwenyekiti wa Mkutano huo wa Kongano Bunifu la Mwani Zanzibar kutoka Wizara ya Kazi Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Vijana Wanawake Watoto na Wazee, Afisa Mkuu wa Uratibu wa Programu za Uwezeshaji, Bi Zeyana Ahmed Kassim akiongoza Mkutano huo katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo Maruhubi uliowashirikisha Wakulima wa Mwani na Wanunuzi wa Makampuni ya Mwani Zanzibar.
Katibu wa Mkutano huo akiwasilisha Dondo za Mkutano uliopita wa Kongano Bunifu la Mwani kwa Wajumbe wa Mkutano huo wa Pili uliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Kilimo Maruhubi Zanzibar.
Mshiriki wa Kongmaano Bunifu la Mwani Zanzibar kutoka Jumuiya ya Wafanyabiashara Zanzibar Dk Mohammed Hafidh akichangia wakati wa mkutano huo wa Kongamano la Mwani Zanzibar.
Naibu Katibu Mkuu wa iliokuwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dk Omar Amir akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa Kongano Bunifu la Mwani Zanzibar.lililowashirikisha Wakulima wa Mwani na Wanunuzi wa Zao la Mwani Zanzibar.
Afisa Mtafiti Mkuu wa Tume ya Taifa Sayansi na Tekohama Zanzibar Dkt Afua Mohammed, akizungumza na Ida StadenbergMwanafunzi kutoka Chuo cha Royar Institute of Technology Sweden na Dan Neren kutoka Sweden, wakimsikiliza Dk Afua wakati wa mapumziko ya mkutano huo wa Kongano Bunifu la Mwani Zanzibar. No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.