Habari za Punde

Rais wa Zanzibar Dk Shein Ateuwa Makatibu Wakuu Zanzibar.

HABARI MAELEZO 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, leo amefanya uteuzi wa viongozi katika Wizara mbalimbali za serikali.

Katika uteuzi huo unaoanza leo tarehe 18 Aprili, 2016.
Mhe. Rais amemteua Dk. Abdulhamid Yahya Mzee kuwa Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi.

Ndg.Salum Maulid Salum anakuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, wakati Naibu wake ni Salmin Amour Abdulla.

Katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Katibu Mkuu ni Radhia Rashid Haroub, na Kai Bashir Mbarouk anakuwa Naibu Katibu Mkuu.
Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Katibu Mkuu ni Asha Ali Abdulla, Naibu Katibu Mkuu anaeshughulikia masuala ya Utumishi wa Umma ni Yakout Hassan Yakout.

Aidha, Kubingwa Mashaka Simba ameteuliwa kuwa Naibu Katibu ofisi hiyo anaeshughulikia masuala ya Katiba, Sheria na Utawala Bora.

Katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Joseph Abdulla Meza anakuwa Katibu Mkuu, Naibu wake ni Ahmed Kassim Haji.


Dk. Shein amemteua Khamis Mussa Omar kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, wakati Ali Khamis Juma ameteuliwa kuwa Naibu wa Wizara hiyo.

Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko, Katibu Mkuu ni Bakari Haji Bakari, wakati Dk. Juma Malik Akili anakuwa Katibu Mkuu katika Wizara ya Afya, Naibu wake ni Halima Maulid Salum, na Dk. Jamala Adam Taib anakuwa Mkurugenzi Mkuu.

Khadija Juma Bakari ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, na Abdulla Mzee ni Naibu anaeshughulikia masuala ya Mipango na Uendeshaji, wakati Madina Mjaka Mwinyi anakuwa Naibu Katibu Mkuu-anaeshughulikia Taaluma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira ni Ali Khalil Mirza, wakati Juma Ali Juma anakuwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Maliasili, Uvuvi na Mifugo, na naibu wake ni Maryam Juma Abdulla.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto ni Fatma Gharib Bilal, wakati Maua Makame Rajab anakuwa Naibu Katibu Mkuu.

Mheshimiwa Rais pia amemteua Omar Hassan Omar kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, na Naibu Katibu Mkuu ni Dk. Amina Ameir Issa.

Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji, Mustafa Aboud Jumbe ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu, wakati Naibu ni Shomari Omar Shomari.
Kwa mujibu wa Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, viongozi wote hao wanatakiwa kufika Ikulu kesho saa 8:30 mchana tayari kwa kuapishwa.    

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.