Habari za Punde

Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Azindua Mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoani Morogoro leo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwasha  Mwenge wa Uhuru kuzindua rasmi mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2016 leo Aprili 18, 2016  sherehe iliyofanyika katika uwwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro. Kulia ni Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa Jmii, Vijana, Wanawake na Watoto -  Zanzibar Mhe. Moudeline Castiko.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi Mwenge wa Uhuru kiongozi wa mbio za Mwenge kwa mwaka 2016  George Jackson Mbijima kutoka mkoa wa Mbeya kwa ajili ya kukimbiza mwenge huo katika Mikoa na wilaya zote za Tanzania.




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia Taifa kwenye Sherehe za uzinduzi wa Mwenge wa Uhuru kitaifa zilizofanyika leo april 18, 2016 katika Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro.
(Picha na OMR)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.