Habari za Punde

Taarifa kwa vyombo vya habari

DW kutengeneza video zenye habari kwa Kiswahili


Idhaa ya Kiswahili ya DW imeanzisha huduma mpya: Mukhtasari 

wa habari ndani ya sekunde 100. Mbali na kukuletea matangazo ya 

redio ya kila siku kwa ajili ya Afrika Mashariki na eneo la Maziwa 

Makuu, Jumatatu hadi Ijumaa DW itakupatia video fupi zenye 

habari. Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili, Andrea Schmidt, ana furaha 

kwamba yeye na timu yake ya waandishi wa habari kutoka nchi 

tano tofauti wanaanzisha huduma hii mpya itakayoitwa Papo kwa 

Papo na itakayokuwa jicho la kuutazama ulimwengu. Kupitia 

video zetu utaweza kupata habari muhimu za kimataifa za kila siku.

“Papo kwa Papo” itapatikana katika chaneli ya YouTube ya DW 

Kiswahili, Facebook na toleo fupi la sekunde 60 litarushwa kupitia 

WhatsApp.


Miongoni mwa mambo mengine, tutakuletea “hashtag” zilizovuma 

pamoja na katuni za kisiasa kutoka kwa wasanii maarufu Gado na 

Said Michael.


Pamoja na hayo, kila Ijumaa DW Kiswahili itakuletea sekunde 100 

za matukio muhimu ya kisiasa yaliyotokea katika juma zima.
· 
  Tafadhali kuwa shabiki wetu YouTube: www.youtube.com/kiswahili
·Jiunge nasi katika ukurasa wetu wa Facebook: https://www.facebook.com/dw.kiswahili.
·        
Pata “Papo kwa Papo” na taarifa zaidi kupitia WhatsApp. Unaweza 
kujiunga nasi kupitia kiungo hiki: bit.ly/1Q86kjt

Kila siku Idhaa ya Kiswahili ya DW inarusha masaa matatu ya 

matangazo Afrika Mashariki na katika eneo la Maziwa Makuu. 

Kwa kushirikiana na redio washirika katika eneo zima, DW 

inawapatia wasikilizaji habari zisizoegemea upande wowote 

kuhusu yanayojiri duniani kwa ujumla na hasa barani Afrika 

kupitia masafa ya FM. Ili kutoa mtazamo huu wa kimataifa, timu 

ya waandshi wa habari kutoka nchi tano inafanya kazi na mtandao 

mkubwa wa waandishi walioko Afrika na kwengineko.

Matangazo ya Kiswahili ni miongoni mwa matangazo ya DW 

yenye wasikilizaji wengi zaidi. DW inajumuisha vipindi 

vilivyopokea tuzo kama vile Learning by Ear - Noa bongo, jenga 

maisha yako - na vipindi vinavyojadili afya, haki za binadamu, 

mazingira, wanawake na maendeleo, vijana na utamaduni na sanaa.

www.dw.com/kiswahili


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.