Habari za Punde

Mjane wa Marehemu Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere Atembelea Daraja la Nyerere Kigamboni Dar es Salaam.

Mama Maria Nyerere, Mjane wa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, 
akiwa na mwanae Mhe. Makongoro Nyerere na msaidizi wake akifurahia mandhari wakati walipotembelea Daraja la Nyerere Kigamboni jijini Dar es salaam.
Mama Maria, ambae hakujali mvua kubwa iliyokuwa inanyesha, alionekana mwenye furaha kufika darajani hapo kwani ndoto ya miaka 
mingi iliyoanzishwa na hayati mumewe imetimia. Pia alimshukuru sana Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwa kuagiza daraja lipewe jina 
la Mwalimu na siyo yeye, jambo ambalo amesema limemfariji sana kwani vizazi vya sasa na nvijavyo vitamkumbuka mwasisi wa Taifa..
(Picha na Ikulu)No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.