Habari za Punde

Waziri Aboud Awatembelea Wananchi Wanaokaa katika Kambi ya Maafa Skuli ya Mwanakwerekwe C Unguja.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohammed Aboud Mohammed akitembelea Kambi ya Wananchi waliopata Maafa ya Mvua za Masika katika Skuli ya Mwanakwerekwe C Unguja kuona maendeleo ya kambi hiyo ikiwa na Wananchi wanaopata hifadhi katika kambi hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Mohammed Aboud Mohammed akisalimiana na baadhi ya Watoto wanaoishi katika Kambi hiyo ya Skuli ya Mwenakwerekwe C Zanzibar.
Waziri Aboud akiwafariji watoto wanaoishi katika kambi hiyo wakati alipofika kuwatembelea na kujua hali za wananchi wanaoishi kambi kambi hiyo.Baadhi ya Watoto waliopata maafa katika makaazi yao wakiwa katika Kituo hicho wakicheza mpira, kama walipovyokutwa na mdau wa blog hii akiwa katika matembezi yake mitaani.
Baadhi ya Watoto wanaoishi katika Kambi ya Skuli ya Mwanakwerekwe C Unguja wakiwa katika mchezo wao kituoni hapo wakicheza mpira. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.