Habari za Punde

Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Balozi Ali Karume Afanya Ziara Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar.

Kamishna wa Zmamoto Zanzibar Ali Mwalimussi akitowa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Balozi Ali Karume wakati wa ziara yake kutembelea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume kujionea utendaji wa Taasisi zinazotowa huduma katika Uwanja huo.
Mawaziri Balozi Ali Karume wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Mhe Haji Omar Kheri wakimsikiliza Kamishna wa Jeshi la Zimamoto Zanzibar akitowa maelezo wakati wa ziara hiyo katika ukumbi wa Ofisi za Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar Kiembesamaki Zanzibar. 
Wakuu wa Idara zinazotowa huduma katika Uwanja wa Ndege wa Zanzibar wakiwa katika ukumbi wa mkutano na Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Balozi Ali Karume.
Waheshimia wakiaza ziara yao katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar. Balozi karume akifuatana na Waziri Mhe Haji Omar Kheri.
Naibu Kamishna wa Kikosi cha Zimamoto Zanzibar Haji Gora Haji akitowa maelezo kwa Waziri Balozi Karume utendaji wa Kikosi chake cha Zimamoto uwanja hapo wakati wa ziara yake kutembelea Uwanja huo.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar Captain Said akitowa maelezo wakati wa ziara ya Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Balozi Ali Karume katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Mhe Haji Omar Kheri akitowa maelezo wakati wa ziara hiyo ya Balozi Karume   
Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Balozi Ali Karume akimsikiliza Meneja Ufundi wa Viwanja vya Ndege Zanzibar Mzee Abdalla wakati wakitembelea uwanja huo wakiwa katika gari maalum ilioandaliwa kutembelea uwanja huo na Watendaji wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar.

Balozi Ali Karume akiagana na Waziri Mwezake baada ya kumaliza ziara yao kutembelea Uwanja wa Ndege wa Zanzibar.
Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafarishaji Balozi Ali Karume akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza ziara yake.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.