Habari za Punde

Dk Shein amuapisha Katibu Mkuu mpya wa Ofis ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein leo amemuapisha Radhia Rashid Haroub kuwa Katibu Mkuu   Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] {15/05/2016.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein akimkabidhi hati ya kiapo Bi,Radhia Rashid Haroub baada  yakumuapisha  rasmin leo  kuwa Katibu Mkuu   Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ leo  katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] {15/05/2016.
Bi,Radhia Rashid Haroub baada  ya kumuapisha  rasmin leo  kuwa Katibu Mkuu   Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SM,[Picha na Ikulu.] {15/05/2016.

STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
 Zanzibar                                  15.5.2016
---
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein leo amemuapisha Radhia Rashid Haroub kuwa Katibu Mkuu   Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ.

Hafla ya kumuapisha Katibu Mkuu huyo ilifanyika Ikulu Mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.


Miongoni mwa viongozi hao ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Haji Gavu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais  Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Haji Omar Kheir.

Wengine ni Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said, Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali, Mkuu wa  Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis, Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Khatib Abrahman Khatib, Wakuu wa Vikosi vya SMZ, Washauri wa Rais wa Zanzibar na viongozi wengine wa Serikali.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.