Habari za Punde

Mzuri Modern Clinic kutoa huduma ya uchunguzi wa afya bila ya malipo

Mzuri Modern Clinic inatangaza siku 3 za uchunguzi wa afya bure kuanzia Jumaatano Mei 11 mpaka Ijumaa Mei 13 kutoka Saa 2 asubuhi mpaka Saa 3 usiku kila siku.

Fursa hii ya muda mfupi bila malipo ni kwa ajili ya watu wote wanaoishi Mjini Zanzibar na mashamba.

Wakati wa zoezi hili, wafanyakazi wa afya waliobobea na uwezo mkubwa watakupima uzito na presha yako na kukupa ushauri wa kitaalmu juu ya afya yako.

Huduma hii itatolewa Mzuri Modern Clinic, Jitini -Miembeni, karibu na makazi ya Sheha wa Shehia ya Miembeni.

Mzuri Modern Clinic inathamini na kujali afya yako. Tunatoa huduma za afya kamilifu.

Meneja Mtendaji

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.